China iko tayari kufanya kazi na Brazil ili kupanua zaidi ushirikiano wa jumla wa China-Latini Amerika: Wang Yi

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Juni 03, 2026

Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi, ambaye pia ni mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), akiongoza Mazungumzo ya Kimkakati ya Tano ya Mawaziri wa Mambo ya Nje wa China na Brazil kwa pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje wa Brazil Mauro Vieira, Beijing, mji mkuu wa China, Juni 1, 2026. (Xinhua/Dai Tianfang)

BEIJING - Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi amesema China wakati wote imekuwa rafiki wa kuaminika wa nchi za Latini Amerika na Karibiani na iko tayari kufanya kazi na nchi za kanda hiyo, ikiwemo Brazil, ili kuzidisha na kupanua ushirikiano wa jumla wa China na Latini Amerika.

Wang, ambaye pia ni mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), ameyasema hayo Jumatatu wiki hii kwenye Mazungumzo ya Kimkakati ya Tano kati ya Mawaziri wa Mambo ya Nje wa China na Brazil na Waziri wa Mambo ya Nje wa Brazil Mauro Vieira mjini Beijing.

Wang amesema kwamba katika miaka ya hivi karibuni, chini ya mwongozo wa kimkakati wa viongozi wakuu wa nchi hizo mbili, uhusiano kati ya China na Brazil umekuwa wa kimataifa, kimkakati na wenye ushawishi mkubwa.

"Ushirikiano wa kivitendo katika nyanja zote umeboreshwa kwa kasi tulivu, na watu wa nchi hizo mbili hawajawahi kuwa karibu zaidi kiasi hicho," ameongeza.

Wang amesema pande hizo mbili zinapaswa kutekeleza kikamilifu maafikiano muhimu yaliyofikiwa na viongozi hao wakuu wawili wa nchi, kuendelea kusukuma mbele ujenzi wa jumuiya ya China na Brazil yenye mustakabali wa pamoja, kukabiliana kwa pamoja na changamoto mbalimbali za nje, na kujenga ushirikiano mkubwa zaidi kwa ajili ya harakati za mambo ya kisasa za kila mmoja na umoja na kujiboresha kwa nchi za Kusini ya Dunia.

Akibainisha kuwa China inathamini ahadi ya muda mrefu ya serikali ya Brazil kwa kanuni ya kuwepo kwa China moja, Wang amesema China inaunga mkono Brazil katika kulinda mamlaka yake huru ya kitaifa, kushikilia uhuru na kujiamulia mambo, na kufikia maendeleo makubwa zaidi.

“Pande hizi mbili zinapaswa kusukuma mbele mabadilishano na ushirikiano katika utamaduni, elimu, utalii, michezo, maeneo ya ngazi za serikali za mitaa, vijana, vyombo vya habari na nyanja zingine,” Wang amesema, akiongeza kuwa ni muhimu kuimarisha mawasiliano na uratibu chini ya mifumo ya pande nyingi ikiwemo Umoja wa Mataifa na BRICS, kutekeleza kwa bidii mapendekezo makuu manne ya kimataifa, na kuhimiza maendeleo ya mfumo wa usimamizi duniani ulio wa haki na usawa zaidi.

Kwa upande wake Vieira amesema kwamba Brazil itafuata kanuni ya kuwepo kwa China moja kila wakati. Amesema Brazil inatarajia kuimarisha kuaminiana kimkakati na China, kuzidisha ushirikiano wa kivitendo, kuimarisha uungwaji mkono wa umma kwa uhusiano wa pande mbili, na kufikia ustawi wa pamoja.

Akibainisha kuwa Brazil na China zote ni nguvu muhimu zinazotetea ushirikiano wa pande nyingi na biashara huria, Vieira amesema Brazil iko tayari kufanya kazi na China ili kuongeza uratibu wa pande nyingi, kusukuma mbele kwa pamoja mageuzi ya mfumo wa utawala duniani, kutetea mamlaka ya Umoja wa Mataifa, na kuhimiza haki na usawa kimataifa.

Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi, ambaye pia ni mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), akiongoza Mazungumzo ya Kimkakati ya Tano ya Mawaziri wa Mambo ya Nje wa China na Brazil kwa pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje wa Brazil Mauro Vieira, Beijing, mji mkuu wa China, Juni 1, 2026. (Xinhua/Dai Tianfang)

Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi, ambaye pia ni mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), akiongoza Mazungumzo ya Kimkakati ya Tano ya Mawaziri wa Mambo ya Nje wa China na Brazil kwa pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje wa Brazil Mauro Vieira, Beijing, mji mkuu wa China, Juni 1, 2026. (Xinhua/Dai Tianfang)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha