Timu ya wataalamu wa matibabu wa China yawasili DRC kuunga mkono makabiliano dhidi ya Ebola

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Juni 03, 2026

Wajumbe wa timu ya wataalamu wa China wa mapambano dhidi ya janga la ugonjwa wakiwasili Kinshasa, mji mkuu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Juni 2, 2026. (Xinhua)

Wajumbe wa timu ya wataalamu wa China wa mapambano dhidi ya janga la ugonjwa wakiwasili Kinshasa, mji mkuu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Juni 2, 2026. (Xinhua)

KINSHASA - Timu ya wataalamu wa China wa mapambano dhidi ya janga la ugonjwa imewasili Kinshasa, mji mkuu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), jana Jumanne kwa ajili ya jukumu la miezi mitatu ya kuunga mkono nchi hiyo ya Afrika ya Kati kukabiliana na mlipuko wa Ebola.

Luku Maleyo Marius, mwakilishi wa Wizara ya Afya ya DRC, aliikaribisha timu hiyo kwenye uwanja wa ndege, akisema kwamba China kupeleka wataalamu wa matibabu kuja nchi hiyo ni kutoa uungaji mkono wenye nguvu kwa wakati kwa serikali ya DRC na watu wake.

“Kila wakati DRC inapokabiliwa na changamoto kubwa za afya ya umma, China imekuwa ikitoa msaada kwa wakati,” amesema, akiongeza kuwa anatarajia utekelezaji wa jukumu hilo la timu ya China utaimarisha zaidi uwezo wa nchi hiyo wa kuzuia, kudhibiti na kutibu ugonjwa, na kusaidia kudhibiti mlipuko huo wa ugonjwa mapema iwezekanavyo.

Lu Ming, mkuu wa timu hiyo ya wataalamu wa China, amesema timu hiyo itaanza kazi haraka kwa kufuata mahitaji ya upande wa DRC na itashirikiana na taasisi za matibabu na za udhibiti wa magonjwa za nchini humo ili kutoa uungaji mkono katika tathmini ya janga, usimamizi wa hali ya wagonjwa, na maeneo mengine.

Ameongeza kuwa timu hiyo itashirikiana kwa karibu na upande wa DRC ili kulinda maisha na afya ya watu, kuchangia ujuzi na utaalamu wa China katika kuisaidia DRC kudhibiti mlipuko huo wa ugonjwa katika kipindi cha mwanzo.

Mei 15, DRC ilithibitisha rasmi mlipuko wake wa 17 wa Ebola tokea mwaka 1976. Siku mbili baadaye, Shirika la Afya Duniani liliutangaza mlipuko huo kuwa tukio la dharura la afya ya umma linalohitaji umakini na ufuatiliaji kimataifa.

Kamati ya Kitaifa ya Afya ya China ilitangaza Jumatatu wiki hii uamuzi wa kutuma timu hiyo ya wataalamu wa matibabu ili kuunga mkono juhudi za kuzuia na kudhibiti Ebola za DRC.

Kamati hiyo ya China imejulisha kuwa, timu hiyo ya kwanza imeundwa na wataalamu watano wenye uzoefu mkubwa katika kuzuia na kudhibiti ugonjwa. Pia watachangia maarifa yao ya kukabiliana na janga kutokana na hali za sehemu husika za huko na kusaidia kuongeza uwezo wa DRC katika kuzuia, kudhibiti na kutibu Ebola. 

Lu Ming (Kushoto), mkuu wa timu ya wataalamu wa China, akizungumza na Luku Maleyo Marius, mwakilishi wa Wizara ya Afya ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Kinshasa, mji mkuu wa DRC, Juni 2, 2026. (Xinhua)

Lu Ming (Kushoto), mkuu wa timu ya wataalamu wa China, akizungumza na Luku Maleyo Marius, mwakilishi wa Wizara ya Afya ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Kinshasa, mji mkuu wa DRC, Juni 2, 2026. (Xinhua)

(Wahariri wa tovuti:Liu Mengxue,Zhao Jian)

Picha