Lugha Nyingine
Mashine ya umeme ya kuinua na kupanga mizigo iliyoundwa China yazinduliwa Tanzania

Picha hii ikionyesha mashine ya umeme inayokabidhiwa hivi karibuni ya kuinua na kupanga mizigo iliyoundwa China ikiinua kontena jijini Dar es Salaam, Tanzania, Juni 1, 2026. (Xinhua/Lin Guangyao)
DAR ES SALAAM –Mashine ya umeme ya kuinua na kupanga mizigo iliyoundwa China imekabidhiwa rasmi jijini Dar es Salaam, Tanzania Jumatatu wiki hii, ikimaanisha zana hiyo ya kutumia nishati mpya kwa ajili ya usambazaji wa bidhaa imeingia katika soko la Tanzania na kuendesha kazi kwa mara ya kwanza.
Mashine hiyo imenunuliwa na Azam Inland Container Depot, kampuni tanzu ya Kundi la Bakhresa. Ali Mukadam, ofisa mtendaji mkuu wa kundi hilo, amesema kuwa uwekezaji huo unaonyesha dhamira yao katika uendeshaji bora na ukuaji endelevu.
"Kwa kutumia teknolojia ya kijani, tunaongeza tija na usalama wakati huohuo tukipunguza utoaji hewa chafu na matumizi ya nishati," Mukadam amesema.
Akizungumza kwenye hafla ya kuzinduliwa kwa mashine hiyo jijini Dar es Salaam, Li Yu, meneja mkuu wa kanda ya Afrika katika kampuni muundaji wa mashine hizo zinazotumia umeme, Guangxi LiuGong Machinery, amesema kuingiza mashine hiyo ni hatua muhimu ya kuhimiza mpango wa kutumia teknolojia za kijani na za AI katika sekta ya usafirisha bidhaa barani Afrika.
Amesema, kampuni hiyo tayari imeleta mashine za umeme za uchimbaji, mashine za kupakia za magurudumu na malori ya shughuli za uchimbaji madini barani Afrika, ili kuunga mkono kanda ya Afrika kuelekea maendeleo ya kutoa kaboni chache.
Jackline Wikechi, ofisa wa usimamizi wa mazingira katika Baraza la Taifa la Usimamizi wa Mazingira la Tanzania, amesema kwamba serikali ya Tanzania inaunga mkono maendeleo ya teknolojia za kijani, zenye kutoa kaboni chache na miradi ya kuhifadhi mazingira. Ameongeza kuwa zana na mashine za umeme za hali ya juu zaidi zinakaribishwa katika soko la Tanzania ili kuhimiza maendeleo endelevu.

Picha hii ikionyesha mashine ya umeme inayokabidhiwa hivi karibuni ya kuinua na kupanga mizigo iliyoundwa China ikiinua kontena jijini Dar es Salaam, Tanzania, Juni 1, 2026. (Xinhua/Lin Guangyao)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



