Makubaliano kati ya Iran na Marekani yaleta matumaini, lakini migawanyiko mikubwa bado yaendelea kuwepo

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Juni 16, 2026

Picha hii iliyopigwa kwa simu ya mkononi ikionyesha meli za kibiashara zilizokwama kwenye maji ya Mlango-Bahari wa Hormuz, karibu na Khasab, mji mdogo kaskazini mwa Oman, Mei 29, 2026. (Xinhua/Wen Xinnian)

CAIRO - Marekani na Iran zimefikia hati ya makubaliano (MoU) ili kumaliza uhasama, kuondoa kizuizi cha Mlango-Bahari wa Hormuz, na kusimamisha operesheni za kijeshi katika maeneo mbalimbali ya vita.

Makubaliano hayo yaliyotangazwa mapema jana Jumatatu, ambayo yamekuwa yakisubiriwa kwa muda mrefu kwa kuwa mgogoro huo wa miezi mitatu unaendelea kuvuruga minyororo ya usambazaji bidhaa duniani na kuathiri masoko ya fedha, yameleta mwanga wa matumaini ya kumalizika kwa mapigano na kurudi kwa utulivu katika eneo hilo.

Hata hivyo, wataalam wanasema kwamba kulingana na maelezo yaliyotolewa hadi sasa, makubaliano hayo hayatatui kimsingi tofauti za muda mrefu kati ya Marekani na Iran juu ya masuala kama vile mpango wa nyuklia, wala hayapunguzi kutoaminiana kati ya pande hizo mbili. Amani ya kudumu katika Mashariki ya Kati, wanasema, inabaki kuwa mbali kufikiwa.

Picha hii iliyopigwa Aprili 7, 2026 ikionyesha mwonekano wa Ikulu ya White House, Washington, D.C., Marekani. (Xinhua/Li Rui)

Picha hii iliyopigwa Aprili 7, 2026 ikionyesha mwonekano wa Ikulu ya White House, Washington, D.C., Marekani. (Xinhua/Li Rui)

Makubaliano hayo yamefikiwa punde tu wakati mivutano katika eneo hilo ilikuwa ikipamba moto kwa mara nyingine tena. Siku ya Jumapili alasiri, Israeli, licha ya tahadhari za awali za Iran, ilifanya shambulizi lingine dhidi ya Beirut, kufuatia shambulizi lake la awali dhidi ya mji mkuu huo wa Lebanon.

Mashambulizi hayo yalisababisha hali mbaya zaidi ya mapigano kati ya Marekani na Iran tangu Aprili, yakisababisha matishio mapya ya kulipiza kisasi kutoka Tehran.

Picha hii iliyopigwa Juni 12, 2026 ikionyesha raia akikagua majengo yaliyobomolewa baada ya shambulizi la hivi karibuni la anga la Israeli, Tyre, Lebanon. (Picha na Ali Hashisho/Xinhua)

Picha hii iliyopigwa Juni 12, 2026 ikionyesha raia akikagua majengo yaliyobomolewa baada ya shambulizi la hivi karibuni la anga la Israeli, Tyre, Lebanon. (Picha na Ali Hashisho/Xinhua)

Huku nchi za kikanda zikikabiliwa na athari mbaya za mgogoro huo wa Marekani na Israeli dhidi ya Iran, makubaliano hayo yamefungua fursa ya amani.

"Makubaliano kati ya Marekani na Iran yatapunguza kimsingi hatari ya mapigano ya moja kwa moja ya kijeshi katika moja ya maeneo muhimu zaidi duniani," amesema Oytun Orhan, mtafiti mwandamizi katika Kituo cha Utafiti wa Mashariki ya Kati chenye makao makuu yake Ankara.

“Kiuchumi, hatua ya namna hiyo inaweza kuwa na matokeo chanya ya kusambaa zaidi ya nchi hizo mbili,” Orhan amesema, akiongeza kuwa kupungua kwa mivutano kutasaidia kutuliza masoko ya nishati, kuwezesha biashara ya baharini, na kuchochea uwekezaji katika eneo pana zaidi la Mashariki ya Kati.

Tathmini yake hiyo imeungwa mkono na wataalamu wengine wa kikanda.

Picha hii iliyopigwa Juni 12, 2026 ikionyesha majengo yaliyoharibiwa baada ya shambulizi la hivi karibuni la anga la Israeli, huko Tyre, Lebanon. (Picha na Ali Hashisho/Xinhua)

Picha hii iliyopigwa Juni 12, 2026 ikionyesha majengo yaliyoharibiwa baada ya shambulizi la hivi karibuni la anga la Israeli, huko Tyre, Lebanon. (Picha na Ali Hashisho/Xinhua)

Hata hivyo Abdulaziz Alshaabani, mtafiti katika Kituo cha Utafiti wa Kisiasa na wa Kimkakati cha Al Riyadh nchini Saudi Arabia amesema ingawa makubaliano hayo yamefikiwa, hiyo haimaanishi kwamba mitafaruku mikubwa kati ya pande hizo mbili imetatuliwa," amesema.

Amesema kuwa tofauti kubwa zinaweza kubaki juu ya mpango wa nyuklia wa Iran, vikwazo, Mlango-Bahari wa Hormuz, na masuala mapana zaidi ya usalama wa kikanda.

(Wahariri wa tovuti:Liu Mengxue,Zhao Jian)

Picha