Wang Yi asema Ufilipino lazima ifanye maamuzi sahihi wakati huu ambapo uhusiano wa pande mbili uko njia panda

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Julai 23, 2026

Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi, ambaye pia ni mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), akikutana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Ufilipino Ma. Theresa Lazaro, huko Manila, Ufilipino, Julai 22, 2026. (Xinhua/Guo Yige)

Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi, ambaye pia ni mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), akikutana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Ufilipino Ma. Theresa Lazaro, huko Manila, Ufilipino, Julai 22, 2026. (Xinhua/Guo Yige)

MANILA – Jana Jumatano waziri wa mambo ya nje wa China Wang Yi alipokutana na waziri wa mambo ya nje wa Ufilipno Ma. Theresa Lazaro huko Manila Ufiliino alisema, uhusiano kati ya China na Ufilipino sasa uko kwenye njia panda, na uhusiano huo utafuata njia gani baadaye utatokana na Ufilipino kufanya maamuzi sahihi na ya busara.

Waziri huyo wa China ameelezea vilivyo msimamo wa makini wa China kwa upande wa Ufilipino na akitoa upingaji mkali juu ya vitendo vya kihatari vya askari wa Ufilipino vya kugonga meli za utekelezaji wa sheria za China kwenye kisiwa cha Ren'ai Jiao.

Wang, ambaye pia ni mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), amesema kwamba uhusiano kati ya China na Ufilipino siku zote ulikuwa umekabiliwa na matatizo na changamoto zisizoisha katika miaka kadhaa iliyopita, ni wazi kwamba hali hii hailingani na maslahi ya upande wowote na pia inazuia maendeleo ya Ufilipino yenyewe.

Amesema pande zote mbili zinapaswa kulinda kwa pamoja amani na maendeleo yaliyopatikana si rahisi katika eneo hilo, hata hivyo, amesema, Ufilipino inaelekea upande tofauti na nchi nyingine za kikanda, na kujifanya kuwa chanzo cha kuharibu amani na utulivu wa kikanda.

"Ukweli wa mambo umethibitisha kwamba kuruhusu nguvu za nje kuingilia mambo ya kikanda na kuvumisha kwa makusudi migogoro ya baharini kunaweza tu kuifanya Ufilipino kuwa chesi inayochezeshwa na wengine," Wang amesema, akiongeza kuwa kitendo chochote cha uchochezi kinachoungwa mkono na nje ya nchi hatimaye kitaifanya tu Ufilipino ione cha mtema kuni.

Wang amesema kwamba China siku zote inajikita katika kushughulikia migongano na kutuliza hali ya mambo kwa kupitia mazungumzo na mashauriano kati ya pande mbili.

Amesema hata hivyo, Ufilipino iliacha mfumo wa mazungumzo wa pande mbili, ikaunda "baraza la usuluhishi" la muda lililoanzishwa kwa kuhimizwa na nguvu za nje ya nchi, na kutengeneza uwongo wa ati upatanisho na kuuvumisha, ambao ni wa kinyume cha sheria na usioweza kufanya kazi.

Lazaro amesema kwamba Ufilipino na China zina historia ndefu ya mawasiliano, siku zote kila moja ni jirani wa nyingine, na hali hii itaendelea daima.

"Ufilipino inaendelea kufuata sera ya kuwepo kwa China moja na kufuata ahadi zake za kidiplomasiazilizotolewa wakati wa hali ya kawaida ya uhusiano wa pande mbili. Kuna China moja tu duniani, na Taiwan ni sehemu isiyotengeka ya China." amesema.“

Lazaro pia amesema upande wa Ufilipino unatumai kutatua matatizo ya mambo ya baharini kwa kupitia mazungumzo na kupata maendeleo katika kuboresha uhusiano wa pande mbili.

(Wahariri wa tovuti:Liu Mengxue,Zhao Jian)

Picha