Lugha Nyingine
Iran yaonya kuzuia usafirishaji wa mafuta na kujibu mapigo kama Marekani itashambulia miundombinu
Kamandi kuu ya kijeshi ya Iran, Makao Makuu ya Khatam al-Anbiya, imeonya Jumatano kwamba kama Marekani ikishambulia miundombinu ya Iran, itazuia usafirishaji wote wa mafuta kutoka Asia Magharibi na kulenga miundombinu ya mafuta, gesi, umeme, na ya kiuchumi katika eneo hilo.
Onyo hilo katika taarifa kwa vyombo vya habari iliyotangazwa na vyombo vya Iran limekuja kutokana na tishio jipya la Rais wa Marekani Donald Trump la "kushambulia" madaraja na mitambo ya umeme ya Iran.
Katika ujumbe wake wa Jumatano uliochapishwa kwenye mtandao wa Truth Social, Trump alisema shambulio lolote la Iran dhidi ya meli katika Mlango-Bahari wa Hormuz litasababisha mashambulizi ya Marekani kwenye daraja moja au kinu cha kufua umeme, ikiwemo vile vilivyo karibu na, au ndani ya mji mkuu Tehran.
Akijibu tishio hilo la Trump, Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Seyed Abbas Araghchi amesema katika ujumbe wake wa Jumatano kwenye mtandao wa X, kwamba “kanuni yetu ya ulinzi iko wazi: jicho kwa jicho. Uchokozi wowote dhidi ya Iran, ukiwemo wa miundombinu, utalazimu jibu lenye nguvu kali na thabiti.”
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



