Lugha Nyingine
Wakimbizi zaidi ya 500 wa Rwanda warejeshwa nyumbani kutoka DRC
Mamlaka husika zimesema wakimbizi zaidi ya 500 wa Rwanda wamerejeshwa nyumbani Jumatano kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (RDC).
Meya wa wilaya ya Rubavu nchini Rwanda Prosper Mulindwa amesema, watu takriban 400 waliorejeshwa nyumbani wameingia Rwanda kupitia mpaka wa pamoja katika wilaya hiyo ya Rubavu.
Watu hao wamepelekwa hadi Kituo cha Mapokezi cha Nyarushishi huko Rusizi nchini Rwanda kabla ya kujumuishwa tena ndani ya jamii zao.
Wakati huohuo, Meya wa wilaya ya Rusizi ya Rwanda Phanuel Sindayiheba amesema, mapema siku hiyohiyo, wakimbizi 108 wa Rwanda wakiwemo watoto 70 pia wamerejeshwa nyumbani kutoka DRC kupitia mpaka wa pamoja huko Rusizi.
Shirika la Kuhudumia Wakimbizi la Umoja wa Mataifa (UNHCR) linaunga mkono jitihada za kuwarejesha nyumbani watu hao na kujumuika tena katika jamii, na kuwasaidia kujenga upya maisha na kuungana tena na familia zao.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



