Lugha Nyingine
UN yasema Ukosefu wa usalama unaendelea kuathiri juhudi za kukabiliana na mlipuko wa Ebola nchini DRC
Ukosefu wa usalama unaendelea kuathiri shughuli za kibinadamu katika Jimbo la Kivu Kaskazini nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), ikiwa ni pamoja na juhudi za Umoja wa Mataifa za kukabiliana na mlipuko huo wa Ebola unaoendelea.
Akiongea jana Jumatano katika mkutano wa kila siku na waandishi wa habari, msemaji wa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa, Stephane Dujarric, amesema kwa mujibu wa mashirika ya kiraia ya jimbo hilo, watu wasiopungua 30 wameuawa na wengine 12 kujeruhiwa katika mashambulizi mfululizo yaliyotokea kwenye eneo la Beni jimboni humo kati ya Julai 13 na 19, na kwamba vurugu hizo zimefanya raia kukimbia makazi yao na kuzuia ufikiaji wa misaada ya kibinadamu katika maeneo yaliyoathiriwa.
Akiinukuu Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Uratibu wa Masuala ya Kibinadamu OCHA, Dujarric amesema, kutokana na hali mbaya ya usalama, mashirika sita ya kibinadamu, wakiwemo washirika wanaosaidia mapambano dhidi ya Ebola, wamesitisha mijongeo yao katika maeneo kadhaa ya Beni.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



