Mahakama ya Marekani yapanga kesi ya Rais wa Venezuela Maduro kuanza kusikilizwa Juni 2027

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Julai 23, 2026

Wafuasi wa Rais wa Venezuela Nicolas Maduro wakiandamana nje ya mahakama jijini New York, Marekani, Julai 22, 2026. (Xinhua/Zhang Fengguo)

Wafuasi wa Rais wa Venezuela Nicolas Maduro wakiandamana nje ya mahakama jijini New York, Marekani, Julai 22, 2026. (Xinhua/Zhang Fengguo)

NEW YORK – Kesi ya Rais wa Venezuela Nicolas Maduro na mkewe Cilia Flores itaanza kusikilizwa rasmi kuanzia Juni 1, 2027, jaji wa Marekani ameamua Jumatano.

Wawili hao, ambao walikana mashtaka ya biashara haramu ya dawa za kulevya na silaha, walifika mahakamani kwa mara ya tatu jijini New York baada ya kukamatwa kwa nguvu na wanajeshi wa Marekani katika uvamizi wa kijeshi mapema Januari mwaka huu.

Katika kikao hicho cha mahakama cha dakika 15 jana Jumatano, Jaji Alvin Hellerstein alipanga tarehe hiyo kuwa ya kuanza kusikilizwa kwa kesi kwa ombi la mawakili wa pande zote mbili.

Wakili wa Maduro, Barry Pollack, amesema atapinga kwanza mashtaka hayo kwa misingi ya kinga ya mamlaka huru ya kitaifa kwa sababu kama hilo litafanikiwa, Maduro hatalazimika kuendelea na kesi hiyo.

Januari 3 mwaka huu, vikosi vya Jeshi la Marekani vilianzisha mashambulizi makubwa dhidi ya Venezuela na kumkamata Maduro na mkewe kwa nguvu kabla ya kuwasafirisha hadi New York. Mashambulizi hayo ya Marekani yaliishtua jumuiya ya kimataifa, hali ambayo ilisababisha mfululizo wa matamko ya kulaani na wasiwasi mkubwa duniani kote.

Alipofikishwa mahakamani kwa mara ya kwanza Januari 5, Maduro alikana mashtaka yote ya Marekani dhidi yake, ikiwemo biashara ya dawa za kulevya.

Wawili hao wamekuwa wakizuiliwa katika jela kwenye Kituo cha Magereza cha Metropolitan huko Brooklyn, New York, tangu walipokamatwa jijini Caracas.

Waandamanaji walikusanyika siku hiyo ya Jumatano nje ya mahakama ya Manhattan yenye ulinzi mkali, wakidai kuachiliwa huru mara moja kwa Maduro na kupinga aina yoyote ya uingiliaji kati wa kijeshi wa Marekani nje ya nchi.

Allison Gunderson, mwandamanaji kutoka Minneapolis, ameliambia Shirika la Habari la China, Xinhua kwamba Marekani inamshtaki rais wa taifa lenye mamlaka huru baada ya kumteka nyara kinyume cha sheria.

"Si haki na ni uhalifu," Gunderson amesema.

Wafuasi wa Rais wa Venezuela Nicolas Maduro wakiandamana nje ya mahakama jijini New York, Marekani, Julai 22, 2026. (Xinhua/Zhang Fengguo)

Wafuasi wa Rais wa Venezuela Nicolas Maduro wakiandamana nje ya mahakama jijini New York, Marekani, Julai 22, 2026. (Xinhua/Zhang Fengguo)

Msafara wa magari ulimsafirisha Rais wa Venezuela Nicolas Maduro na mkewe Cilia Flores ukiondoka kwenye mahakama ya New York katika Jiji la New York, Marekani, Julai 22, 2026. (Xinhua/Liu Yanan)

Msafara wa magari ulimsafirisha Rais wa Venezuela Nicolas Maduro na mkewe Cilia Flores ukiondoka kwenye mahakama ya New York katika Jiji la New York, Marekani, Julai 22, 2026. (Xinhua/Liu Yanan)

Msafara wa magari uliombeba Rais wa Venezuela Nicolas Maduro na mkewe Cilia Flores ukiondoka kwenye mahakama ya New York katika Jiji la New York, Marekani, Julai 22, 2026. (Xinhua/Liu Yanan)

Msafara wa magari uliombeba Rais wa Venezuela Nicolas Maduro na mkewe Cilia Flores ukiondoka kwenye mahakama ya New York katika Jiji la New York, Marekani, Julai 22, 2026. (Xinhua/Liu Yanan)

Wafuasi wa Rais wa Venezuela Nicolas Maduro wakiandamana nje ya mahakama jijini New York, Marekani, Julai 22, 2026. (Xinhua/Zhang Fengguo)

Wafuasi wa Rais wa Venezuela Nicolas Maduro wakiandamana nje ya mahakama jijini New York, Marekani, Julai 22, 2026. (Xinhua/Zhang Fengguo)

(Wahariri wa tovuti:Liu Mengxue,Zhao Jian)

Picha