AU yaonya mashambulizi ya Wahouthi katika Bahari ya Sham ni tishio kwa usalama wa kikanda

(CRI Online) Julai 24, 2026

Umoja wa Afrika (AU) Alhamisi umelaani vikali mashambulizi yanayodaiwa kufanywa na kundi la Wahouthi la Yemen dhidi ya meli za kibiashara za mafuta katika Bahari ya Sham, ukionya kwamba vitendo hivyo vinawakilisha kupamba moto kwa hali ya hatari kwenye athari kubwa kwa amani na usalama wa kikanda.

Katika taarifa, Mwenyekiti wa Kamisheni ya AU Mahmoud Ali Youssouf ameelezea mshikamano kamili na Saudi Arabia akisisitiza tena "uungaji mkono usioyumba wa Umoja huo kwa usalama, uhuru, na utulivu" wa nchi hiyo.

Youssouf amesisitiza kwamba mashambulizi dhidi ya meli za kibiashara na jaribio lolote la kuzuia mijongeo huru ya vyombo vya usafiri baharini "ni tishio kubwa kwa usalama wa baharini wa kimataifa na kwa utulivu wa moja ya njia za maji za kimkakati zaidi duniani."

Ametoa wito kwa kundi hilo la Houthi "kusitisha mara moja mashambulizi yote dhidi ya meli za kibiashara, kujiepusha na hatua yoyote ambayo inaweza kufanya mivutano kupamba moto zaidi, na kuheshimu kikamilifu sheria ya kimataifa inayosimamia usafiri wa baharini."

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha