Mradi wa maji uliojengwa na Kampuni ya China wabadilisha maisha katika mji kame wa Kenya

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Julai 24, 2026

Picha iliyopigwa Julai 14, 2026 ikionyesha matangi ya kuhifadhi maji kwenye Kiwanda cha Kutibu Maji cha Marsabit, kituo cha kisasa cha kusambaza maji kilichojengwa na Kampuni ya Ujenzi wa Umeme ya China, Marsabit, Kenya. (Xinhua/Liu Qiong)

NAIROBI – Muda wa jioni, kituo cha maji cha jamii katika mji wa Marsabit, kaskazini mwa Kenya, kinakuwa na pilika nyingi wakati ambapo wakazi wanakuwa wakifika na ndoo za njano kuchota maji. Baadhi huja kwa miguu, wakati wengine hupanda pikipiki kusafirisha maji nyumbani.

Hali hiyo hutofautiana sana na wakati uliopita, wakati uhaba wa maji ulitawala maisha ya kila siku katika mji huo.

"Nilikuwa nikiondoka nyumbani saa kumi na mbili asubuhi na wakati mwingine sikurudi hadi jioni," anakumbushia Hawo Hussein, mkazi mwenyeji na mmiliki wa duka dogo la samosa, akiongeza kuwa hata baada ya kusubiri kwenye foleni siku nzima, hakukuwa na uhakika kwamba angepata maji yoyote.

"Sasa ninaweza kuchota maji baada ya dakika chache, na hiyo inamaanisha muda zaidi kwa biashara yangu na familia yangu," amesema.

Mji wa Marsabit, uliopo katika ardhi kame na nusu kame ya Kenya, hupata mvua kidogo, na ile inayonyesha mara nyingi hupotea haraka kwenye miteremko. Wakati wa misimu mirefu ya kiangazi, familia zilitegemea maji ya ardhini na mabwawa ya msimu ambayo mara nyingi hayakuwa ya kutosha kukidhi mahitaji.

Leo, taswira hiyo inabadilika. Mfumo wa kisasa wa kusambaza maji uliojengwa na Kampuni ya Ujenzi wa Umeme ya China umeleta maji safi na ya kuaminika kwa mji huo na jamii zinazozunguka, hali ambayo imerahisisha moja ya changamoto za maendeleo za muda mrefu zaidi katika eneo hilo.

Mradi huo uliozinduliwa mwaka 2023 na kukabidhiwa kabisa kwa Kenya mwaka 2025, unajumuisha bwawa, kituo cha kusukuma maji, kiwanda cha kutibu maji, mabomba ya usafirishaji na mtandao wa usambazaji, na kujenga mfumo jumuishi kuanzia kuhifadhi maji hadi kuyasambaza kwenye kaya.

Kwa mujibu wa Zhang Yang, naibu meneja wa mradi huo wa maji, Bwawa la Bakuli No. 4 lililojengwa hivi karibuni limepanua uwezo wa bwawa kuhifadhi maji mara tano hadi mita za ujazo takriban 250,000, na kuwezesha mji huo kuvuna maji ya mvua chache za msimu na kuhimili vyema miezi ya ukame.

Stanley Kamande, kamishna wa Kaunti ya Marsabit, amesema hifadhi ya maji iliyopo inaweza kukidhi mahitaji ya mji huo kwa takriban miezi sita chini ya viwango vya sasa vya matumizi, akiongeza kuwa kufuatia maji ya kutosha kuwa ya uhakika, changamoto inayofuata ilikuwa kuyafikisha salama kwenye makazi ya wakazi.

Bomba la usafirishaji linalounganisha kituo hicho kipya cha kusukuma maji na kiwanda cha kutibu maji lililazimika kuvuka matuta 27 ya milima, huku baadhi ya miteremko ikikaribia nyuzi 60, na kufanya iwe vigumu kwa mashine nzito kufikia sehemu fulani.

"Katika maeneo magumu zaidi, vifaa vya ujenzi vililazimika kusafirishwa na punda na kubebwa kwa mikono hadi kwenye maeneo ya kazi," Zhang amesema.

Bomba hilo lililokamilika sasa linasambaza maji kote mjini, na kuleta maboresho halisi katika maisha ya kila siku ya wakazi.

Mkazi mwenyeji akijaza vyombo vya maji kwenye sehemu ya kuchotea maji ya umma iliyojengwa na Kampuni ya Ujenzi wa Umeme ya China, Marsabit, Kenya, Julai 14, 2026. (Xinhua/Liu Qiong)

Mkazi mwenyeji akijaza vyombo vya maji kwenye sehemu ya kuchotea maji ya umma iliyojengwa na Kampuni ya Ujenzi wa Umeme ya China, Marsabit, Kenya, Julai 14, 2026. (Xinhua/Liu Qiong)

Picha iliyopigwa Julai 14, 2026 ikionyesha Bwawa la Bakuli No. 4 lililojengwa hivi karibuni katika Hifadhi ya Taifa ya Marsabit, Kenya. (Xinhua/Liu Qiong)

Picha iliyopigwa Julai 14, 2026 ikionyesha Bwawa la Bakuli No. 4 lililojengwa hivi karibuni katika Hifadhi ya Taifa ya Marsabit, Kenya. (Xinhua/Liu Qiong)

Picha iliyopigwa Julai 14, 2026 ikionyesha jengo la ofisi ya Kampuni ya Huduma za Maji ya Kaunti ya Marsabit, iliyojengwa na Kampuni ya Ujenzi wa Umeme ya China, Marsabit, Kenya. (Xinhua/Liu Qiong)

Picha iliyopigwa Julai 14, 2026 ikionyesha jengo la ofisi ya Kampuni ya Huduma za Maji ya Kaunti ya Marsabit, iliyojengwa na Kampuni ya Ujenzi wa Umeme ya China, Marsabit, Kenya. (Xinhua/Liu Qiong)

(Wahariri wa tovuti:Liu Mengxue,Zhao Jian)

Picha