Lugha Nyingine
Makamu Rais wa Uganda aipongeza kongani ya viwanda ya ushirikiano wa kilimo inayoungwa mkono na China kwa kuhimiza mabadiliko ya muundo wa kilimo

Makamu Rais wa Uganda Jessica Alupo (katikati) akikagua bidhaa ya nanasi iliyofungashwa kwenye kopo wakati wa kutembelea kwenye Kongani ya Viwanda ya Ushirikiano wa Kilimo kati ya China na Uganda katika Wilaya ya Luwero, Uganda, Julai 23, 2026. (Picha na Hajarah Nalwadda/Xinhua)
LUWERO, Uganda - Makamu Rais wa Uganda Jessica Alupo ameipongeza Kongani ya Viwanda ya Ushirikiano wa Kilimo kati ya China na Uganda kwa kuwa msukumo muhimu kwa mabadiliko ya muundo wa kilimo ya nchi hiyo kwa kupitia utengenezaji wa mazao ya kilimo.
Alupo ametoa pongezi hizo jana Alhamisi wakati alipoongoza ujumbe wa maofisa waandamizi wa serikali kwenye ukaguzi wa kongani hiyo ya viwanda katika wilaya ya Luwero katikati mwa Uganda.
"Ziara ya leo imeonesha vilivyo ahadi ya Uganda katika kuufanyia mabadiliko ya muundo wa uchumi wetu kwa kupitia maendeleo ya viwanda mahsusi vya kilimo," amesema. "Lengo letu la kimkakati liko wazi: kubadilisha sekta yetu ya kilimo kutoka kuwa kilimo cha kijadi cha kujitosheleza hadi kuwa kilimo cha kisasa cha kibiashara chenye nyongeza kubwa ya thamani."
Alupo ameupongeza mpango wa Ushirikiano wa FAO-China-Uganda Kusini-Kusini, ambao chini yake kongani hiyo ya viwanda inayoongozwa na sekta binafsi ya China ilianzishwa, akisema kwamba umeiwezesha Uganda kufanya utengenezaji wa mazao ya kilimo kwa ajili ya kusafirishwa kuuzwa duniani.
Ameahidi kwamba serikali ya Uganda itaendelea kuboresha na kuunga mkono ujenzi wa miundombinu na sera na hatua ili kusukuma mbele maendeleo ya kongani hiyo na kujenga mazingira yanayoweza kusaidia zaidi uwekezaji wa kilimo na viwanda.
Mwaka huu ni maadhimisho ya miaka 10 tangu kuanzishwa kwa kongani hiyo, katika eneo hili kuna kiwanda cha makopo ya nanasi, kiwanda cha utoaji wa pilipili kavu kwa ajili ya kutengenezwa nchini China, pamoja na shamba la kuku wa kutaga mayai linalosambaza mayai kwa masoko ya Uganda na ya kikanda.
“Uganda itanufaika zaidi na ufunguaji mlango wa kigezo cha juu wa China na sera yake ya ushuru-sifuri kwa mauzo ya nje yanayostahiki,” amesema Alupo. "Tunatarajia kuongeza mauzo zaidi ya nje kwa kupitia kutumia ipasavyo sera ya ushuru-sifuri kwa asilimia 100."
Luo Heng, mkurugenzi mkuu wa Kampuni ya Maendeleo ya Viwanda ya Kehong Tawi la Uganda, ambayo ni kampuni ya China inayosimamia kongani hiyo ya viwanda, amesema kazi ya kipindi cha kwanza cha kuanzishwa kwa eneo hilomwaka 2016 imekamilika, ikihusisha miradi mikubwa ya kilimo cha kibiashara cha kuku wa kutaga mayai, kilimo cha pilipili, usindikaji wa nanasi, na uenezi wa aina za mpunga wa mbegu bora.
Luo amesema kongani hiyo inapanga kuwekeza dola milioni 500 za Marekani katika miaka mitano ijayo kuwa kazi ya sehemu moja ya kipindi cha pili cha maendeleo ya eneo hilo.

Makamu Rais wa Uganda Jessica Alupo akizungumza baada ya kutembelea kwenye Kongani ya Viwanda ya Ushirikiano wa Kilimo kati ya China na Uganda katika Wilaya ya Luwero, Uganda, Julai 23, 2026. (Picha na Hajarah Nalwadda/Xinhua)

Picha iliyopigwa Julai 23, 2026 ikionesha kiwanda cha kusindika nanasi kwenye Kongani ya Viwanda ya Ushirikiano wa Kilimo kati ya China na Uganda katika Wilaya ya Luwero, Uganda. (Picha na Hajarah Nalwadda/Xinhua)

Picha iliyopigwa Julai 23, 2026 ikionesha shamba la kibiashara la kuku wa kutaga mayai kwenye Kongani ya Viwanda ya Ushirikiano wa Kilimo kati ya China na Uganda katika Wilaya ya Luwero, Uganda. (Picha na Hajarah Nalwadda/Xinhua)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



