Lugha Nyingine
Sudan yasema asilimia 75 ya vituo vyake vya afya vimeanza tena kufanya kazi
Waziri wa Afya wa Sudan Bw. Haitham Mohamed Ibrahim, amesema, hospitali na vituo vya msingi vya afya karibu asilimia 75 vya nchi hiyo vimeanza tena kufanya kazi baada ya uharibifu mkubwa uliotokana na vita, na dola za Marekani milioni 293 za ufadhili wa kimataifa zimepatikana ili kuunga mkono ufufuaji wa sekta hiyo.
Akizungumza jana Jumapili katika mkutano na waandishi wa habari mjini Khartoum, Bw. Ibrahim amesema, ingawa juhudi wakati wa vita zilijikita katika huduma za dharura, mwenendo wa sasa unaashiria mabadiliko kuelekea kujenga upya mfumo wa afya, hasa baada ya wizara hiyo kurejea katika mji mkuu.
Amesema kuwa mpango huo wa kujenga upya, unaoitwa "Mkakati wa Matumaini," kwa uungwaji mkono kutoka Shirika la Afya Duniani (WHO), unatarajiwa kuzinduliwa Jumatano wiki hii, ukilenga kuimarisha huduma za afya ya msingi na kitaalamu nchini kote.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



