Xi asema China iko tayari kuimarisha zaidi uratibu wa kimkakati na Brazil ulio wa pande mbili na pande nyingi

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Julai 28, 2026

BEIJING - Rais wa China Xi Jinping jana Jumatatu katika mazungumzo kwa njia ya simu na Rais wa Brazil Luiz Inacio Lula da Silva amesema kuwa China iko tayari kuimarisha zaidi uratibu wa kimkakati na Brazil ulio wa pande mbili na pande nyingi.

Xi amesema katika miaka ya hivi karibuni, ujenzi wa jumuiya ya China na Brazil yenye mustakabali wa pamoja na kuhusiana kwa mikakati ya maendeleo ya nchi hizo mbili kumepata maendeleo ya kuhimiza juhudi, ambayo imefanya kazi muhimu katika kusukuma mbele maendeleo ya nchi hizo mbili na kuongeza ustawi wa watu wa pande hizo mbili, wakati huohuo ikichangia utulivu wa thamani kwa hali ya msukosuko ya kimataifa.

Xi amesema kwamba, kwa kukabiliwa na hali mpya na changamoto mpya, China na Brazil, zote zikiwa wajumbe muhimu wa kundi la nchi za Dunia ya Kusini, zinapaswa kusimama kithabiti kwenye upande sahihi wa kihistoria, vilevile kusimama kwenye upande wa maendeleo ya ustaarabu, na kufanya kazi kubwa zaidi ya kiujenzi katika kuufanyia mageuzi na kukamilisha mfumo wa usimamizi wa Dunia, na kushikilia haki na usawa wa kimataifa.

Xi amesema, China inatilia maanani sana nafasi ya Brazil duniani na ushawishi wake muhimu, na inaiunga mkono Brazil katika kulinda mamlaka ya nchi na uhuru wake, kupinga uingiliaji wa nje, na kuchangia katika kudumisha amani na utulivu wa kikanda na dunia.

Lula amesema Brazil na China zimepata maendeleo ya kuhimiza juhudi katika kujenga Dunia yenye usawa zaidi na kujenga jumuiya yenye mustakabali wa pamoja ili sayari ya Dunia iwe na maendeleo endelevu zaidi, ambapo maendeleo ya ushirikiano katika sekta mbalimbali yanasukumwa mbele kwa kasi.

Amesema biashara ya pande mbili imefikia kiwango kipya cha juu cha kihistoria, wakati huohuo mfululizo wa shughuli zilizofanyika wakati wa Mwaka wa Utamaduni wa Brazil na China zimeimarisha zaidi msingi wa kiumma kwa urafiki kati ya watu wa nchi hizo mbili.

Lula ameongeza kwa kusema, "Brazil iko tayari kuongeza uratibu na China kwa pande nyingi, kushikilia mamlaka na heshima ya Umoja wa Mataifa, kuimarisha mshikamano na ushirikiano kati ya nchi za BRICS, kulinda kithabiti ushirikiano wa pande nyingi, kupinga kithabiti siasa za nchi kubwa zenye nguvu kutoa shinikizo kwa nchi dhaifu na ndogo, kufuata utatuzi wa masuala ya migogoro kupitia mazungumzo na mashauriano, na kwa pamoja kulinda haki na usawa wa kimataifa na amani na utulivu wa dunia."

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha