China yatoa wito kwa pande zote za mgogoro wa Ukraine kudumisha mawasiliano na kufikia usimamishaji mapigano haraka

(CRI Online) Julai 28, 2026

Kaimu Balozi wa China katika Umoja wa Mataifa Sun Lei amesema hali ya sasa nchini Ukraine inatia wasiwasi kwani mgogoro unazidi kupamba moto kwa kasi na ametoa wito kwa mwelekeo huo wa hatari kubadilishwa haraka iwezekanavyo.

Akizungumza Jumatatu kwenye mkutano wa wazi wa dharura juu ya mgogoro wa Ukraine wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, Balozi Sun amesema China inatoa wito kwa pande zote kudumisha mawasiliano, kuwa na dhamira ya kisiasa, kuongeza kuaminiana kupitia mazungumzo, kujenga maafikiano kupitia mazungumzo, na kujitahidi kufikia makubaliano ya amani kamili, ya kudumu, na shirikishi.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha