Lugha Nyingine
Trump atishia kufanya “vitendo vya kijeshi vyenye nguvu” kama mazungumzo na Iran yatashindwa

Watu wakishiriki kwenye shughuli ya mazishi ya Kiongozi Mkuu wa Iran Ali Khamenei, Mashhad, Iran, Julai 9, 2026. (Xinhua/Shadati)
WASHINGTON - Rais wa Marekani Donald Trump amesema kwamba ameamua kusitisha kwa muda upigaji makombora kutoka angani dhidi ya Iran ili kutoa fursa nyingine ya mazungumzo, wakati huohuo ameonya kwamba kama mazungumzo hayo na Iran yatashindwa huenda atatoa amri ya kuanzisha tena upigaji makombora.
Jana kwenye mahojiano na chombo cha habari cha mtandaoni cha Marekani Axio, Trump alisema, "Tuko kwenye mazungumzo ya kina sana na Iran. Kama hayatafanikiwa, tutarudi kwenye vitendo vya kijeshi vyenye nguvu kubwa."
Alipoulizwa ni muda gani anaopenda kutoa kwa mbinu ya kidiplomasia, amesema, "Hakuna muda mwingi. Ama mazungumzo yatatatua matatizo kwa haraka, au hakuna muda kabisa kwa mbinu ya kidiplomasia."
Trump amesema aliamua kusitisha kwa muda upigaji makombora siku ya Ijumaa iliyopita kwa sababu nchi zinazopatanisha pamoja na nchi nyingine katika eneo hilo zote zilimtaka kuyapa mazungumzo na Iran fursa nyingine.
Baadaye, rais huyo aliwaambia waandishi wa habari kwamba Iran inaweza tu kutafuta mazungumzo mara tu baada ya jeshi lake kupigwa pigo kali na jeshi la Marekani.
Trump alipokuwa ndani ya Air Force One njiani kuelekea Michigan alisema, "Nadhani kuna uwezekano mkubwa wa kutokea kwa baadhi ya mambo. Na kama mambo hayo yatatokea, ni vizuri, kama hayatatokea, tutarudi kufanya kile tulichokuwa tukifanya siku mbili zilizopita."
Trump amesema kwamba serikali yake na serikali ya Israeli "ziko karibu sana" na maoni ya kauli moja katika suala la Iran.
Alipomtaja waziri mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahu, Trump alisema, "Tuna maoni tofauti kidogo, lakini uhusiano wetu ni wa karibu sana," Benjamin Netanyahu, ambaye anatarajiwa kuzuru Ikulu ya White House leo Jumanne (kwa saa za Marekani).
Trump pia amesisitiza kwamba mali za Iran zinazodhibitiwa na Marekani zitatumika kufidia hasara za meli zilizoshambuliwa wakati zikipita kwenye Mlango-Bahari wa Hormuz. "Tutatumia pesa za Iran kulipa hasara zilizosababihwa nayo," amesema.
Habari nyingine zilizonukuu ripoti ya vyombo vya habari vya kikanda zikisema kuwa, mazungumzo kati ya Oman na Iran yamepata maendeleo, ingawa hazijafikia makubaliano.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



