Lugha Nyingine
Sudan Kusini yaanzisha kampeni ya kuelimisha wapiga kura kwa ajili ya uchaguzi wa Desemba
(CRI Online) Julai 28, 2026
Tume ya Taifa ya Uchaguzi ya Sudan Kusini (NEC) imeanzisha kampeni ya kuelimisha wapiga kura na raia kote nchini jana Jumatatu, ili kufanya maandalizi kwa ajili ya uchaguzi mkuu utakaofanyika tarehe 22 Desemba, hatua ambayo ni sehemu ya jitihada za maandalizi kwa ajili ya uchaguzi wa kwanza wa kitaifa nchini humo tangu nchi hiyo ilipojipatia uhuru mwaka 2011.
Mwenyekiti wa NEC Abednego Akok Kacuol amesema, kampeni hiyo inalenga kuelimisha watu wenye sifa ya kupiga kura juu ya mchakato wa kujiandikisha na kupiga kura, vilevile haki za raia, na kuhamasisha ushiriki kote nchini.
(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



