Lugha Nyingine
Mkutano wa UN wafunguliwa nchini Kenya kutathmini malengo ya bioanuwai
Mkutano wa siku 6 ulioandaliwa chini ya Mkataba wa Umoja wa Mataifa juu ya Bioanuwai (UN CBD) umeanza Jumatatu wiki hii katika mji mkuu wa Kenya, Nairobi, kutathmini upigaji hatua duniani kuelekea malengo 23 yaliyowekwa mwaka 2022 chini ya Mfumo wa Dunia wa Bioanuwai wa Kunming-Montreal.
Mkutano huo wa 28 wa Chombo Tanzu juu ya Ushauri wa Kisayansi, Kiufundi na Kiteknolojia (SBSTTA-28) umekutanisha wajumbe wa CBD kwa lengo la kutathmini mikakati inayolenga kuzuia na kurudisha nyuma upotevu wa spishi ifikapo mwaka 2030.
Wakati wa mkutano huo, washiriki watajadili vipaumbele muhimu, ikiwemo uhifadhi wa viumbe vya baharini na pwani, usimamizi wa wanyamapori, na maeneo ya hifadhi, na kuweka msingi kabla ya Mkutano wa 17 wa Pande watia saini wa Mkataba wa Viumbe Anuwai (COP17) utakaofanyika Yerevan, nchini Armenia, mwezi Oktoba mwaka huu.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



