Lugha Nyingine
Xi Jinping afanya mazungumzo na Rais wa Slovakia Peter Pellegrini mjini Beijing

Rais wa China Xi Jinping akifanya mazungumzo na Rais wa Slovakia Peter Pellegrini anayefanya ziara ya kiserikali nchini China, kwenye Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing, Julai 28, 2026. (Xinhua/Li Xiang)
BEIJING - Rais wa China Xi Jinping amefanya mazungumzo na Rais wa Slovakia Peter Pellegrini mjini Beijing jana Jumanne akisema kwamba China inapenda kushirikiana na Slovakia katika kujenga uhusiano wa wenzi wa kimikakati ulio na umaalumu wa kuheshimiana na kuaminiana, kuwa na usawa na kunufaishana, na wa utulivu na uhimilivu.
Xi amesisitiza kwamba kuheshimiana kwa njia za maendeleo ya kila upande mmoja na kuahidi kithabiti kwa urafiki na ushirikiano, huu ni msingi wa ukuaji mzuri na wa haraka wa uhusiano kati ya China na Slovakia.
“China inaipongeza Slovakia kwa kushikilia kanuni ya kuwepo kwa China moja na itaendelea kufanya ushirikiano na Slovakia, ambapo kila upande utatilia maanani zaidi maslahi makuu ya upande mwingine na ufuatiliaji wa upande mwingine juu ya masuala makuu,” amesema.
Ametoa wito wa kutaka nchi hizo mbili kutumia uwezo wa ushirikiano kwa kuendeleza kazi za sekta zinazoibuka na nyanja za mstari wa mbele zikiwa ni pamoja na nishati safi, uchumi wa kidijitali, teknolojia ya roboti na AI, ili kuanzisha mambo mapya katika ushirikiano wa pande mbili.
Xi amesema China na Slovakia zinapaswa kulinda pamoja mfumo wa kimataifa ambao kiini chake ni Umoja wa Mataifa na utaratibu wa kimataifa unaofuata sheria za kimataifa, kuhimiza kwa pamoja dunia ya ncha nyingi yenye usawa na utaratibu na utandawazi wa uchumi wenye manufaa na jumuishi kwa wote, na kuchangia katika kujenga jumuiya ya binadamu yenye mustakabali wa pamoja.
Xi amesema, “China siku zote inauchukulia Umoja wa Ulaya kuwa ni mshirika na inaendeleza uhusiano wake na Umoja wa Ulaya kwa udhati na nia njema,” na akitoa wito kwa Slovakia kufanya kazi ya kiujenzi katika kuhimiza maendeleo mazuri na ya utulivu ya uhusiano kati ya China na Umoja wa Ulaya.
Rais Pellegrini, ambaye yuko katika ziara ya kiserikali nchini China akisema kuwa, Slovakia inatilia maanani sana uhusiano wa wenzi wa kimkakati kati yake na China, na kutarajia matokeo zaidi kwenye ushirikiano katika uchumi na biashara, AI, uchumi wa kidijitali, tekolojia ya roboti na nishati mpya. Ameongeza kuwa Slovakia inakaribisha kampuni zaidi za China kuwekeza nchini humo.
Pellegrini amesema, "Slovakia ikiwa nchi mwanachama wa Umoja wa Ulaya inapenda kufanya juhudi za kuhimiza ushirikiano kati ya Umoja wa Ulaya na China na kuondoa kwa kufaa migongano kwa kupitia mazungumzo na mashauriano".
Kabla ya mazungumzo yao, Xi alifanya hafla ya kumkaribisha Pellegrini. Na mchana ilimwandalia dhifa ya makaribisho.

Rais wa China Xi Jinping akifanya mazungumzo na Rais wa Slovakia Peter Pellegrini, ambaye yuko katika ziara ya kiserikali nchini China, kwenye Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing, Julai 28, 2026. (Xinhua/Yin Bogu)

Rais wa China Xi Jinping akifanya hafla ya kumkaribisha Rais wa Slovakia Peter Pellegrini kwenye Ukumbi wa Kaskazini wa Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing, kabla ya mazungumzo yao, Julai 28, 2026. (Xinhua/Ding Lin)

Rais wa China Xi Jinping akifanya hafla ya kumkaribisha Rais wa Slovakia Peter Pellegrini kwenye Ukumbi wa Kaskazini wa Jumba la Mikutano ya Umma la Beiijing, kabla ya mazungumzo yao, Julai 28, 2026. (Xinhua/Yue Yuewei)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



