Viongozi wa Afrika waeleza wasiwasi juu ya kuanza tena kwa mapigano Mashariki ya Kati

(CRI Online) Julai 29, 2026

Viongozi wa Afrika wameeleza wasiwasi juu ya kuanza tena kwa mapigano katika kanda ya Mashariki ya Kati, ambayo wamesema, yanachochea msukosuko mkubwa wa uchumi na usalama barani Afrika kupitia mishtuko ya nishati, mivurugiko ya ugavi na kupanda kwa bei.

Kauli hiyo imetolewa kwenye Mkutano wa Kawaida wa 49 wa Kamati ya Utendaji ya Umoja wa Afrika jana Jumanne katika makao makuu ya Umoja huo mjini Addis Ababa, Ethiopia.

Akizungumza kwenye mkutano huo, Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika Mahmoud Ali Youssouf amesema, Afrika inabeba mzigo mkubwa zaidi wa mgogoro huo wa Mashariki ya Kati, huku nchi nyingi katika bara hilo zikikabiliwa na gharama kubwa ya maisha kutokana na kupanda kwa bei ya mafuta.

Katibu Mtendaji wa Kamisheni ya Uchumi ya Umoja wa Mataifa kwa Afrika (UNECA) Claver Gatete amesema, mazingira duniani yamezidi kuwa na hali ya kutokuwa na uhakika wakati huu ambapo bei za nishati, chakula na mbolea zikipanda kutokana na mgogoro huo unaoendelea katika Mashariki ya Kati.

(Wahariri wa tovuti:Liu Mengxue,Zhao Jian)

Picha