Lugha Nyingine
Watu zaidi ya milioni 400 barani Afrika wakosa huduma ya maji safi ya kunywa
Katibu Mtendaji wa Kamisheni ya Uchumi ya Umoja wa Mataifa kwa Afrika Bw. Claver Gatete amesema, watu zaidi ya milioni 400 barani Afrika bado wanakosa njia ya kufikia huduma ya msingi ya maji safi ya kunywa, wakati watu zaidi ya milioni 700 katika bara hilo wanapoendelea kutokuwa na mifumo ya usafi inayosimamiwa kwa usalama.
Wakati akihutubia Mkutano wa 49 wa Kawaida wa Baraza la Utendaji la Umoja wa Afrika (AU) Jumanne wiki hii mjini Addis Ababa, mji mkuu wa Ethiopia, Bw. Gatete amesema hali hiyo inaathiri afya, tija, usalama wa chakula na maendeleo ya kiuchumi katika bara hilo.
Akisisitiza kwamba maji yapo katikati ya kila changamoto kubwa ya maendeleo inayoikabili Afrika leo, Bw. Gatete amezihimiza serikali za Afrika kukumbatia mipango shirikishi katika nyanja za maji, kilimo, nishati, tabianchi, viwanda na maendeleo ya miji.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



