Lugha Nyingine
Maafisa watano wa usalama wa Kenya wauawa katika shambulizi linaloshukiwa kufanywa na kundi la al-Shabaab
(CRI Online) Julai 30, 2026
Maafisa watano wa usalama wa Kenya wameuawa Jumanne wiki hii katika shambulizi la kuvizia linaloshukiwa kufanywa na wapiganaji wa kundi la al-Shabaab katika Kaunti ya Mandera karibu na mpaka wa nchi hiyo na Somalia.
Polisi wamesema, shambulizi hilo lilitokea katika eneo la El-Raamo huko Kutulo kwenye Njia Kuu ya Ugavi ya Alungu, wakati gari la maafisa hao lilipokanyaga kifaa cha kulipuka kilichotengenezwa kienyeji (IED) kabla ya kushambuliwa kwa risasi na kusababisha vifo vya maafisa usalama hao.
Mamlaka za usalama zimeanza uchunguzi wa kina kuhusu tukio hilo na zimepeleka maofisa wengine kurejesha usalama katika eneo hilo na kuwasaka wapiganaji hao waliotoroka.
(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



