Bunge la Afrika lahimiza maandalizi thabiti zaidi ya kiafya dhidi ya milipuko

(CRI Online) Julai 30, 2026

Bunge la Afrika (PAP) limetoa wito kwa nchi za Afrika kuongeza uwekezaji katika afya ya umma, kuimarisha ufuatiliaji wa magonjwa na kuongeza kasi ya uzalishaji wa ndani wa chanjo ili kukabiliana na milipuko inayoweza kutokea siku za baadaye.

Mwenyekiti wa Kamati ya Afya, Kazi na Masuala ya Kijamii ya Bunge hilo, Frank Annoh-Dompreh ameyasema hayo jumanne wiki hii wakati wa mjadala wa bunge hilo mjini Johannesburg, Afrika Kusini kuhusu mlipuko wa Ebola barani Afrika.

Amesema nchi za Afrika zinahitaji kuimarisha maandalizi yao kwa dharura za afya za siku za baadaye, akisisitiza umuhimu wa kuboresha usimamizi wa takwimu za afya ya umma na kufanyia mageuzi mifumo ya takwimu za afya ili kukabiliana vizuri na milipuko inayoweza kutokea siku za baadaye.

Amesema mpaka kufikia tarehe 19 mwezi huu, mlipuko wa hivi karibuni wa Ebola umerekodi watu 2,443 waliothibitishwa kuambukizwa, vifo 969, huku wagonjwa 487 wakiwa wamepona.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha