Lugha Nyingine
Maofisa wa UN wahimza kukabiliana kithabiti zaidi na Ebola nchini DRC
Mratibu Mwandamizi wa Ebola wa Umoja wa Mataifa Julien Harneis na kaimu mkurugenzi mtendaji wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) Carl Skau, wametoa wito kwa jumuiya ya kimataifa kuongeza kwa kiasi kikubwa juhudi za kukabiliana na Ebola nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) kwani kusambaa kwa mlipuko huo kumezidi nguvu ya kukabiliana nao.
Maofisa hao wametoa wito huo katika mkutano na wanahabari uliofanyika kwa njia ya mtandao jana Jumatano kutoka Bunia, mji mkuu wa Jimbo la Ituri, ambao ni kiini cha mlipuko huo wa sasa wa Ebola.
Skau amesema, mlipuko huo wa Ebola nchini DRC ni janga la Ebola linalokua kwa kasi zaidi kuwahi kutokea. “Kwa kufanya ulinganifu, katika miezi miwili iliyopita, watu 1,000 wamefariki (nchini DRC). Ilichukua miezi minane kwa watu 1,000 kufariki Afrika Magharibi.” Amesema.
Kwa upande wake Harneis amesema, kasi ya kukabiliana na mlipuko huo lazima iongezwe haraka, kwa ufadhili, mahitaji, timu za madaktari zaidi na uwezekano wa kuwafikia wale wanaohitaji.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



