Lugha Nyingine
Familia ya watu wenye tamaduni tofauti yaunganisha lugha na utamaduni na kuleta mambo zaidi ya kufurahisha maisha ya watoto

Steven Dahlke (wa kwanza, kushoto) na mkewe Gulayim Akim (wa pili, kushoto) kwa kujitolea wakifundisha watoto kujifunza lugha ya Kichina na ya Kiingereza kwenye darasa la majira ya joto katika sehemu moja ya wakazi ya eneo la jengo la biashara huko Urumqi, mji mkuu wa Mkoa Unaojiendesha wa Kabila la Wauygur wa Xinjiang, kaskazini magharibi mwa China, Julai 24, 2026. (Xinhua/Hu Huhu)
Steven Dahlke mwenye umri wa miaka 45 kutoka Rostock nchini Ujerumani amekuwa akiishi na kufanya kazi nchini China kwa miaka mingi. Alikutana na na kupendana na Gulayim Akim, mzaliwa wa Mkoa wa Xinjiang, mwaka 2011. Walianzisha familia yenye furaha mwaka 2015, na wanaishi Urumqi kuanzia mwaka 2022.
Wanandoa hao walikuwa wakishangazwa na kipaji cha lugha cha mtoto wao wa kiume Jacob Steven, waliamua kuanzisha kituo cha kujisomea vitabu vya picha vya lugha ya Kichina na ya Kiingereza ili kusaidia watoto wa wakazi kuongeza ujuzi na kupanua upeo wa macho. Kituo hicho kilifunguliwa na kuanza kutoa huduma katikati ya mji huo wa Urumqi mwaka 2024.
Wanadoa hao wenye uzoefu wa miaka mingi katika elimu ya juu, walitumia uwezo wao wa kujua lugha mbalimbali na kutoa mafunzo kwa njia zinazolenga ukuaji wa watoto, na siku hadi siku wametambuliwa na wakazi wa huko.
Wakati huo huo, wanashiriki kwa bidii katika huduma za kujitolea kwenye eneo la makazi, wakiandaa shughuli za kujisomea za umma wakati wa siku za mapumziko za umma, na wamefanya juhudi za kuhamasisha vizazi vya watoto na vijana kusoma zaidi na kupata ujuzi zaidi.
Uwanja mpya kabisa wa ndege wa kimataifa, usafiri wa ndege unaoongezwa zaidi kuelekea nchi mbalimbali, majengo makubwa ya biashara yanayojengwa zaidi kwa kasi, na maeneo mapya ya kitamaduni yaliyofunguliwa vyote vimemwezesha Dahlke kuhisi kikweli mabadiliko makubwa yaliyotokea katika mji huo wa Urumqi. Machoni mwake, maendeleo hayo ya kasi ya mji huo wa kaskazini magharibi mwa China yametoa uungaji mkono wenye nguvu kwa ukuaji wa huduma yao hiyo ya kujisomea kwa watoto na vijana.
Wanandoa hao pia wana matumaini mazuri juu ya mustakabali wa kazi zao, walisema, "Lugha ni daraja muhimu la kuunganisha dunia, na kujenga urafiki". Wanatumai mawasiliano kati ya watu wanaotumia lugha tofauti yataleta maelewano na upendo kwa kuvuka mipaka.

Steven Dahlke (kushoto) na mkewe Gulayim Akim wakifundisha watoto Kiingereza kwenye kituo chao cha kujisomea huko Urumqi, Mkoa Unaojiendesha wa Kabila la Wauygur wa Xinjiang, kaskazini magharibi mwa China, Julai 22, 2026. (Xinhua/Hu Huhu)

Steven Dahlke (kushoto), Gulayim Akim (kulia) na mtoto wao Jacob Steven (wa pili, kulia) wakitembelea eneo la utamaduni mjini Urumqi, Mkoa Unaojiendesha wa Kabila la Wauygur wa Xinjiang, kaskazini magharibi mwa China, Julai 24, 2026. (Xinhua/Hu Huhu)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



