Kongamano la Kimataifa lafunguliwa Cape Town ili kusukuma mbele viwango vya elimu ya lugha ya Kichina na ujanibishaji wake

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Julai 30, 2026

Ren Faqiang (nyuma), Konsuli Mkuu wa China mjini Cape Town, akizungumza kwenye hafla ya ufunguzi wa kongamano mjini Cape Town, Afrika Kusini, Julai 28, 2026. (Xinhua/Wang Lei)

Ren Faqiang (nyuma), Konsuli Mkuu wa China mjini Cape Town, akizungumza kwenye hafla ya ufunguzi wa kongamano mjini Cape Town, Afrika Kusini, Julai 28, 2026. (Xinhua/Wang Lei)

CAPE TOWN - Kongamano la kimataifa kuhusu elimu ya lugha ya Kichina limefunguliwa Cape Town, Afrika Kusini, Jumanne wiki hii, likiwaleta pamoja wataalamu kujadili maendeleo ya viwango vya elimu ya lugha ya Kichina na ujanibishaji wa ufundishaji.

Kongamano hilo la siku mbili limeandaliwa kwa pamoja na Chuo Kikuu cha Western Cape (UWC), Jumuiya ya Walimu wa Lugha ya Kichina Afrika Kusini, na Kituo cha Utafiti wa Ikolojia ya Lugha cha Ukanda Mmoja, Njia Moja katika Chuo Kikuu cha Ualimu cha Zhejiang, China.

Wataalamu zaidi ya 50 kutoka nchi 13 wanahudhuria kongamano hilo kujadili ufundishaji na ujifunzaji wa lugha ya Kichina, maendeleo ya elimu ya kimataifa ya lugha ya Kichina, mafunzo ya walimu wa ndani, rasilimali za elimu za kidijitali na zenye akili, na usanifishaji wa elimu ya lugha ya Kichina.

Akihutubia hafla ya ufunguzi, Monwabisi Ralarala, kaimu makamu mkuu wa chuo ambaye pia ni naibu makamu mkuu wa Chuo Kikuu cha UWC, amesema kongamano hilo linaambatana na maadhimisho ya miaka 10 tangu Lugha ya Kichina kujumuishwa rasmi katika mtaala wa elimu ya msingi wa Afrika Kusini na "linaadhimisha muongo mmoja wa ushirikiano."

Katika hotuba yake, Konsuli Mkuu wa China mjini Cape Town Ren Faqiang amesema lugha ina jukumu muhimu katika kuhimiza mawasiliano miongoni mwa watu, kuhifadhi ustaarabu mbalimbali, na kuongeza kuelewana.

Amesema elimu ya lugha ya Kichina si tu kwamba inafungua fursa zaidi za maendeleo na ajira kwa vijana wa Afrika Kusini, lakini pia inaimarisha msingi wa uhusiano kati ya watu wa China na Afrika Kusini, na hivyo kuwakilisha ufanyaji dhahiri wa mabadilishano ya kitamaduni na kufunzana kati ya mataifa yetu mawili.

Washiriki wakihudhuria kongamano mjini Cape Town, Afrika Kusini, Julai 28, 2026. (Xinhua/Wang Lei)

(Wahariri wa tovuti:Liu Mengxue,Zhao Jian)

Picha