Rwanda kuwapa majina sokwe wachanga 22 wakati uhifadhi na utalii vikiendelea kukua

(CRI Online) Agosti 12, 2026

Rwanda itawapa majina sokwe 22 wa milimani waliozaliwa katika kipindi cha miezi 12 iliyopita kwenye sherehe za 21 za kila mwaka za Kwita Izina za kuwapa majina sokwe zitakazofanyika Septemba 4 mwaka huu.

Katibu mtendaji wa Mfuko wa Mazingira wa Rwanda Eugene Mutangana ametangaza jana Jumanne kuwa sherehe hiyo itafanyika chini ya vilima vya Hifadhi ya Taifa ya Volkeno katika Wilaya ya Musanze, kaskazini mwa Rwanda.

Kwita Izina limekuwa tukio kubwa la uhifadhi na utalii, likionyesha juhudi za Rwanda za kuwalinda sokwe hao wa milimani, wakati huoho ikiunganisha uhifadhi wa wanyamapori na utalii, maendeleo ya jamii na ukuaji endelevu wa uchumi.

Akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari mjini Kigali, Mutangana amesema sherehe hiyo ya kila mwaka inaakisi imani ya Rwanda kwamba uhifadhi unapaswa kunufaisha mazingira ya asili na watu.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha