Lugha Nyingine
Timu ya matibabu ya China yatoa mafunzo ya matibabu ya jadi ya Kichina kwa wafanyakazi wa afya wa Tanzania
Kundi la 28 la timu ya matibabu ya China kwa Tanzania bara imeendesha kozi yake ya pili ya mafunzo kuhusu matibabu ya jadi ya Kichina (TCM) kwa wafanyakazi wa afya wa msingi wa Tanzania na wataalamu wa afya wa jamii.
Kwa mujibu wa daktari wa TCM katika timu hiyo ya matibabu ya China, Wang Hongqing, mafunzo hayo, yaliyofanyika katika Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni jijini Dar es Salaam siku ya Jumapili, yalijikita katika nadharia za msingi za matibabu ya jadi ya Kichina na ujuzi wa kivitendo wa tiba ya akyupancha, yakiwapatia washiriki maarifa ya nadharia na uzoefu wa vitendo. Daktari Wang pia alitoa mihadhara kuhusu dhana za msingi za matibabu hayo.
Naye mwakilishi wa Jumuiya ya Kuhimiza Urafiki kati ya Tanzania na China, Husna Sharif, ameishukuru timu hiyo ya matibabu, akisema mafunzo hayo ni sehemu ya juhudi pana za kuchangia utaalamu wa kimatibabu na kuimarisha uwezo wa wafanyakazi wa afya wenyeji, ambapo yamechangia ushirikiano wa karibu zaidi wa afya kati ya Tanzania na China na uhusiano baina ya watu wa pande hizo mbili.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



