Idadi ya vifo kwenye ajali ya kupinduka kwa boti nchini Zimbabwe yaongezeka hadi 44 huku hali ya maafa ikitangazwa

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Agosti 13, 2026

Picha iliyopigwa kwa simu ya mkononi ikionyesha waokoaji wakifanya shughuli za utafutaji na uokoaji kwenye eneo la ajali ya boti kupinduka katika Ziwa Kariba, Jimbo la Mashonaland Magharibi, Zimbabwe, Agosti 12, 2026. (Str/Xinhua)

HARARE - Rais wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa ametangaza hali ya maafa jana Jumatano kufuatia kupinduka kwa boti katika Ziwa Kariba, huku polisi wakithibitisha kuwa idadi ya vifo kutokana na janga hilo imeongezeka hadi kufikia 44.

Katika taarifa, Waziri wa Serikali za Mitaa na Ujenzi wa Umma wa Zimbabwe, Daniel Garwe amesema tangazo hilo la rais linaiwezesha serikali kuchukua hatua za dharura na kuratibu rasilimali muhimu ili kusaidia na kulinda watu walioathiriwa au wanaoweza kuathiriwa na janga hilo.

Garwe amesema boti hiyo, ambayo ilikuwa ikisafiri kutoka Kariba hadi Chalala, ilipinduka juzi Jumanne baada ya kuripotiwa kupigwa na mawimbi makali ilipokuwa ikisafiri karibu na Kisiwa cha Long.

Amesema wakati wa tukio hilo, boti hiyo ilikuwa imebeba abiria 114 na wafanyakazi watano. Amesema, idadi isiyojulikana ya watoto pia inaaminika walikuwa ndani yake. Garwe ameeleza kuwa, hadi kufikia sasa (jana Jumatano), watu 77 walikuwa wameokolewa wakati shughuli za utafutaji na uokoaji zikiwa bado zinaendelea.

"Serikali inatoa rambirambi zake za dhati kwa familia na wapendwa wa wale waliopoteza maisha yao katika tukio hili la kusikitisha," Garwe amesema.

Picha iliyopigwa kwa simu ya mkononi ikionyesha manusura wa ajali ya kupinduka kwa boti kwenye Ziwa Kariba wakipata hifadhi katika shule moja katika Jimbo la Mashonaland Magharibi, Zimbabwe, Agosti 12, 2026. (Str/Xinhua)

(Wahariri wa tovuti:Liu Mengxue,Zhao Jian)

Picha