Lugha Nyingine
Kufungua Pazia | Sehemu ya 4: Kwa nini mzee alificha kitufe chake cha kuita kwa dharura?
Maelezo ya Mhariri:
Kipindi cha “Kufungua Pazia” kinatumia simulizi halisi na mazingira ya kila siku kuelezea mantiki ya maendeleo nyuma ya Mpango wa 15 wa Miaka Mitano wa China. Kupitia simulizi za viwandani, watu na mambo halisi yaliyotokea, kinawapa watazamaji duniani mtazamo unaohusiana na kufikika zaidi kuhusu hatua inayofuata ya maendeleo ya China.
Katika sehemu ya 4 ya “Kufungua Pazia,” Mina anapewa kazi ya kuwasha tena kituo cha huduma za utunzaji wazee baada ya mfumo kubainisha hali isiyo kawaida ya kiafya ya mzee mwanamke, aishiye peke yake ambaye kifaa chake cha kuita kwa dharura kimeachwa bila ya kutumia kwa muda mrefu.
Wakati Mina anapochunguza, anatambua kuwa tatizo si kwamba mwanamke huyu hajui namna ya kutumia kifaa hicho au hahitaji uungaji mkono. Ni kwamba ana wasiwasi kuhusu kusumbua familia yake na hataki kuonekana kuwa mtu asiyeweza tena kusimamia maisha yake mwenyewe.
Ufahamu huo unamsaidia Mina kutambua kuwa huduma zilizo rafiki kwa wazee zinakwenda mbali zaidi ya ufuatiliaji wa hali ya afya na usaidizi wa dharura. Zinapaswa kutoa masuluhisho yanayofikika, mahsusi, na angalifu zaidi, ambayo yanakidhi mahitaji mbalimbali ya wazee - kuanzia mashauriano ya kiafya na huduma za chakula hadi uambatanaji wa kihisia, shughuli za kitamaduni na ushiriki kwenye jamii, ili kuwasaidia kuishi maisha salama zaidi, yaliyo rahisi zaidi na ya kuridhisha nafsi.
Mwongozo wa Mpango wa 15 wa maendeleo ya uchumi na jamii ya Miaka Mitano (2026-2030) wa China unatoa wito wa juhudi za kuboresha maisha ya wazee, kuendeleza kwa bidii uchumi wa wazee na kupanua usambazaji wa bidhaa zilizo rafiki kwa wazee na huduma za kutunza wazee.
Maendeleo ya kweli yaliyo rafiki kwa wazee siyo tu kuhusu kuwapa wazee matunzo na ulinzi. Ni kuhusu kuwawezesha kupokea uungaji mkono kwa heshima, kubaki kuwa wameunganishwa na jumuiya zao na kuendelea kutafuta maisha yenye kuridhisha nafsi katika miaka yao ya baadaye.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



