Lugha Nyingine
Hatua za ushuru-sifuri za China zatoa fursa mpya kwa mageuzi ya viwanda ya Nigeria
Utekelezaji wa sera ya ushuru-sifuri ya China kwa mauzo ya nje kutoka nchi za Afrika umeelezwa kuwa tayari unachochea ukuaji katika biashara ya pande mbili na kutoa fursa mpya kwa Nigeria kuongeza kasi ya mageuzi ya viwanda na kupanua mauzo ya nje kwa bidhaa zisizotokana na mafuta.
Hayo yamesemwa na washiriki katika semina ya kimataifa kuhusu “Sera ya Ushuru-Sifuri ya China kwa Asilimia 100 ya Bidhaa Zinazostahiki kutozwa Ushuru kwa Nchi za Afrika na Maana yake Katika Mageuzi ya Muundo wa Uchumi wa Afrika” iliyofanyika katika mji mkuu wa Nigeria, Abuja, Ijumaa wiki iliyopita.
Akizungumza katika semina hiyo, Waziri wa Nchi wa Nigeria anayeshughulikia Kilimo na Usalama wa Chakula Aliyu Sabi Abdullahi ametoa wito kwa marekebisho ya muundo wa ndani ya nchi hiyo, akisema wazalishaji wanapaswa kuhamisha malengo yao kutoka kusafirisha malighafi hadi kusafirisha bidhaa za kilimo zilizoongezwa thamani.
Naye Balozi wa China nchini Nigeria Yu Dunhai amesema, bidhaa kutoka Nigeria zimeongezeka kwenye soko la China tangu kuanza kutekelezwa kwa sera hiyo ya China ya ushuru-sifuri kwa nchi 53 za Afrika zenye uhusiano nayo wa kidiplomasia, wakati huohuo ukuaji wa kila mwezi umezidi asilimia 40 kwa mwezi Mei na Juni.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



