Lugha Nyingine
Kufungua Pazia | Sehemu ya 6: Kwa jinsi gani picha ya kuchorwa ukutani inakwenda nje ya pango?
Maelezo ya Mhariri:
Kipindi cha “Kufungua Pazia” kinatumia simulizi halisi na mazingira ya kila siku kuelezea mantiki ya maendeleo nyuma ya Mpango wa 15 wa Miaka Mitano wa China. Kupitia simulizi za viwandani, watu na mambo halisi yaliyotokea, kinawapa watazamaji duniani mtazamo unaohusiana na kufikika zaidi kuhusu hatua inayofuata ya maendeleo ya China.
Katika sehemu ya 6 ya “Kufungua Pazia,” Mina anakwenda kwenye Kituo cha Maonesho ya Kidijitali cha Mapango ya Mogao huko Dunhuang, Mkoa wa Gansu, China ambako mtembeleaji kijana anashindwa kuingia Pango No. 285 kwasababu nafasi zote zilizomo zimejaa.
Kwa kufuata utepe wa kung’ara kutoka kwenye picha ya kuchorwa ukutani ya apsara anayeruka, Mina anatembea kuingia ndani ya kituo cha utengenezaji wa mapango ya kidijitali. Humo anabaini kuwa utengenezaji huo wa kidijitali unahusu mambo mengi zaidi ya kupiga tu picha za kale za kuchorwa mapangoni. Mchakato huo unahifadhi siyo tu rangi na nakshi zao ndogo ndogo za kina, bali pia mwanga, nafasi na hisia za nyakati ndani ya mapango.
Kwa kupitia maonesho changamani na teknolojia ya VR, watembeleaji wanaweza kuangalia juu kwenye dari lenye sehemu ya katikati inayoinuka (Zao-jing), kukaribia zaidi apsara wanaoruka na hata kuhisi kama wamesafiri kupitia nyakati tofauti kwa kusimama ndani ya pango na kupata mwonekano sawasawa na ule ambao mafundi waliona miaka elfu iliyopita.
Mina anakuja kuelewa kuwa teknolojia haimaanishi kuwa mbadala wa urithi wa awali, badala yake inaupa mabawa, ikiwezesha hazina za kitamaduni zisizoweza kuhamishika kusafiri zaidi ya kwenye mapango, kufikia watu wengi zaidi na kuchochea shauku ya dhati ya kuzilinda.
Mwongozo wa Mpango wa 15 wa Miaka Mitano (2026-2030) wa China unatoa wito wa kufungamanisha zaidi utamaduni na teknolojia, kuwezesha maendeleo ya utamaduni kwa kutumia teknolojia ya kidijitali na bora zaidi ya kisasa, kuhama kuelekea mtindo wa maendeleo wenye kutegemea IT, na kukuza aina mpya za biashara za kiutamaduni.
Njia bora ya kuhifadhi urithi haijawahi kamwe kuwa kuhusu kuugandisha katika zama za kale. Ni kuhusu kuuachilia uvuke miaka elfu ili uongee na watu katika kila zama. Wakati mchoro wa kale ukutani bado unaweza kuvutia macho ya mtu leo hii, hali hiyo ni uthibitisho wa kutosha kuwa nyakati za zamani kamwe hazijapita kiukweli.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



