Lugha Nyingine
Kenya yatarajia China kuchangia uboreshaji wa viwanda vyake

Joseph Mutavi Kithu, mkurugenzi wa kitaifa wa Jumuiya wa Wafanyabiashara na Wamiliki wa Viwanda ya Kenya, akitoa hotuba kwenye Maonesho ya 9 ya Kimataifa ya Viwanda ya Kenya, jijini Nairobi, Kenya, Septemba 3, 2026. (Xinhua/Liu Qiong)
NAIROBI - Kenya itaongeza kwa kina ushirikiano na China ili kuboresha uwezo wake wa viwanda, kuongeza mauzo ya nje ya bidhaa zilizoongezwa thamani, na kutengeneza ajira kwa vijana, maafisa waandamizi wamesema jana Alhamisi kwenye Maonesho ya 9 ya Kimataifa ya Viwanda ya Kenya jijini Nairobi, mji mkuu wa Kenya.
Joseph Mutavi Kithu, mkurugenzi wa kitaifa wa Jumuiya wa Wafanyabiashara na Wamiliki wa Viwanda ya Kenya (KNCCI), jumuiya ya wafanyabiashara, amesema kwamba China inatoa nguvu ya kuwezesha ukuaji ya kimkakati kwa ajili ya ufufuaji wa viwanda wa taifa hilo la Afrika Mashariki.
Kithu ameeleza kwamba uwezo wa hali ya juu wa viwanda wa China, uliojengwa juu ya teknolojia ya kisasa, nguvu kazi yenye ujuzi, na minyororo ya usambazaji ya uhakika, unaweza kuunga mkono maendeleo ya kiviwanda ya Kenya.
"Tutaleta zana nyingi zaidi kutoka China ili sasa tuweze kuanza kuzalisha hapa Kenya," Kithu amesema.
"Pia tunawahamasisha watu wa China kuanzisha biashara hapa kwa sababu wakati unapozalisha hapa, itakuwa rahisi kufikia soko," ameongeza.
Pius Rotich, mkurugenzi wa uwekezaji wa sekta ya viwanda wa Mamlaka ya Uwekezaji ya Kenya (Invest Kenya), amesema katika hafla ya ufunguzi kwamba serikali imeweka mazingira mazuri ya sera na usimamizi ili kuvutia uwekezaji wa China katika viwanda vya ndani, kuongeza mauzo ya nje, na kukabiliana na ukosefu wa uwiano kibiashara.
Rotich amebainisha kuwa mashine za viwandani zinazoagizwa kutoka China zimefanya mistari ya uzalishaji kwa wazalishaji wa ndani kuwa ya kisasa, hali ambayo imeongeza uwezo wa kushindana wa bidhaa za Kenya katika masoko ya kikanda na kimataifa.
Kwa mujibu wa Gao Wei, mkurugenzi mkuu wa Kampuni ya Afripeak Expo Kenya, Maonyesho ya Kimataifa ya Viwanda ya Kenya yamebadilika kupitia hali mbalimbali katika kipindi cha miaka mingi iliyopita kutoka kuwa maonyesho ya kawaida ya biashara hadi jukwaa kubwa la kukuza ushirikiano wa kiviwanda, uwekezaji wa kuvuka-mipaka, na ubadilishanaji wa teknolojia.
Maonyesho hayo yaliyoandaliwa na Kampuni ya Afripeak Expo Kenya na kuandaliwa kwa ushirikiano na KNCCI na Mamlaka ya Uwekezaji ya Kenya (Invest Kenya), yanashirikisha kampuni zaidi 100 za China zinazoonesha uvumbuzi katika viwanda, usafiri wa kijani, huduma ya afya, na ujenzi.

Mtembeleaji akiangalia mashine ya kuchora kwa leza inayooneshwa na kampuni ya China kwenye Maonesho ya 9 ya Kimataifa ya Viwanda ya Kenya jijini Nairobi, Kenya, Septemba 3, 2026. (Xinhua/Liu Qiong)

Mtembeleaji akijaribu pikipiki inayotumia umeme inayooneshwa na kampuni ya China kwenye Maonesho ya 9 ya Kimataifa ya Viwanda ya Kenya jijini Nairobi, Kenya, Septemba 3, 2026. (Xinhua/Liu Qiong)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



