WHO na Kenya kuimarisha hatua za mwitikio wa hali ya hewa ya El Nino

(CRI Online) Septemba 09, 2026

Shirika la Afya Duniani (WHO) linafanya uratibu kwa karibu na serikali ya Kenya kukabiliana na matishio ya kiafya yanayohusiana na msimu ujao wa El Nino wa mwaka 2026/2027.

Akizungumza jana jijini Nairobi kabla ya msimu wa mvua wa Oktoba – Desemba, Mwakilishi wa WHO nchini Kenya Neema Rusibamayila Kimambo amesema, tathmini endelevu za matishio zitatoa mwongozo kwa mamlaka za afya katika kutambua matishio na kuimarisha utayari wa mwitikio dhidi ya mafuriko na milipuko ya magonjwa inayohusiana na mabadiliko ya hali ya hewa.

Katika kukabiliana na hali hiyo, Wizara ya Afya nchini Kenya imeanzisha Mpango wa Sekta ya Afya Kukabiliana na El Nino, ili kutoa mwongozo wa juhudi za kitaifa za utayari na mwitikio wa dharura.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha