Maonesho ya mwanga wa droni yaangaza mabadilishano kati ya watu wa China na Botswana

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Septemba 10, 2026

Droni zikipangiliwa kuonesha tendo la kushikana mikono na Ukuta Mkuu wa China kwenye maonesho ya mwanga wa taa za droni, Gaborone, Botswana, Septemba 8, 2026. (Xinhua/Tshekiso Tebalo)

Droni zikipangiliwa kuonesha tendo la kushikana mikono na Ukuta Mkuu wa China kwenye maonesho ya mwanga wa taa za droni, Gaborone, Botswana, Septemba 8, 2026. (Xinhua/Tshekiso Tebalo)

GABORONE - Maonesho ya mwanga wa taa za droni 500 zilizopangiliwa kwa maumbo maaulum Jumanne usiku wiki hii yalivutia mamia ya watazamaji kwenye Uwanja wa Chuo Kikuu cha Botswana huko Gaborone, mji mkuu wa Botswana, ili kuonesha urafiki na mabadilishano kati ya watu wa China na Botswana.

Maonesho hayo yaliyotanguliwa na ngoma ya simba na dragoni, yalifanywa na mafundi Wachina na yalionesha mfululizo wa taswira angani zinazoonesha mambo vinara na alama za nchi hizo mbili, zikiwa ni pamoja na Ukuta Mkuu wa China, pundamilia, tembo, panda, njiwa wa amani, almasi, Kung Fu, alama ya sarafu ya Botswana PULA na maandishi ya Kichina yanayomaanisha baraka, vilevile ishara ya kushikana mikono, ili kuonesha utamaduni na ushirikiano.

Watazamaji waliwasha taa za simu zao za mkononi huku wakishangilia na kupongeza maonesho, ambayo yaliambatana na muziki na kuangazwa kwa rangi angavu.

Akitoa hotuba kwenye shughuli hiyo, Balozi wa China nchini Botswana Fan Yong, akiwa amevaa miwani ya AI, amesema mwaka huu ni wa maadhimisho ya miaka 70 tangu kuanzishwa uhusiano wa kidiplomasia kati ya China na nchi za Afrika, pia Mwaka wa Mabadilishano Kati ya Watu wa China na Afrika, na unatokea wakati sawa na maadhimisho ya miaka 60 ya uhuru wa Jamhuri ya Botswana.

"Maonyesho haya ya jioni hii ni zaidi ya muunganiko wa kupendeza wa teknolojia na sanaa; pia ni sherehe yenye nguvu hai wa urafiki mkubwa kati ya China na Afrika, China na Botswana," amesema.

Amesifu sana mafanikio ya miaka 51 ya uhusiano wa pande mbili, na ameapa kuendelea kuongeza na kuimarisha ushirikiano wa kimkakati kati ya China na Botswana, ili kuhakikisha unatoa manufaa zaidi na halisi kwa watu wao.

Helen P. Manyeneng, naibu spika wa Bunge la Botswana, ambaye alihudhuria shughuli hiyo, alisikiliza maelezo ya waandaaji wa maonesho hayo akiwa na shauku kubwa katika droni na teknolojia.

Shughuli iliandaliwa na Kundi la Muunganisho wa Vyombo vya Habari vya Radio na Televisheni la Shaanxi, China na Ubalozi wa China nchini Botswana, kwa ushirikiano na Wizara ya Uhusiano wa Kimataifa na Wizara ya Michezo na Sanaa ya Botswana.

Mpangilio wa droni ukionesha tembo na panda kwenye maonesho ya mwanga wa taa za droni, Gaborone, Botswana, Septemba 8, 2026. (Xinhua/Tshekiso Tebalo)

Mpangilio wa droni ukionesha tembo na panda kwenye maonesho ya mwanga wa taa za droni, Gaborone, Botswana, Septemba 8, 2026. (Xinhua/Tshekiso Tebalo)

Mpangilio wa droni ukionesha watu wakifanya Kung Fu ya Kichina kwenye maonesho ya mwanga wa taa za droni, Gaborone, Botswana, Septemba 8, 2026. (Xinhua/Tshekiso Tebalo)

Mpangilio wa droni ukionesha watu wakifanya Kung Fu ya Kichina kwenye maonesho ya mwanga wa taa za droni, Gaborone, Botswana, Septemba 8, 2026. (Xinhua/Tshekiso Tebalo)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha