Lugha Nyingine
Maambukizi ya Ebola yaenea katika mkoa mpya nchini DRC
(CRI Online) Septemba 11, 2026
Mlipuko wa Ebola nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) umeenea na kufika katika mkoa wa Sud-Ubangi ulioko kaskazini magharibi mwa nchi hiyo baada ya kesi moja kuthibitishwa.
Kaimu Gavana wa Sud-Ubangi Jean-Rene Galekwa Vundawe amesema katika taarifa yake iliyotolewa jana, kwamba vipimo vya maabara vimethibitisha virusi vya Ebola aina ya Bundibugyo, na kuzifanya mamlaka kutangaza mlipuko wa ugonjwa huo katika mkoa huo.
Mamlaka hazijaweka wazi chanzo cha maambukizi hayo ama muunganiko wowote unaojulikana kuhusiana na mlipuko wa sasa kwani mkoa wa Sud-Ubangi haupakani na mikoa sita ambako kesi za Ebola ziliripotiwa awali, ambayo ni Ituri, Kivu Kaskazini, Kivu Kusini, Haut-Uele, Tshopo na Bas-Uele.
(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



