Lugha Nyingine
Xi na Modi wabadilishana maoni kwa kina, wakubaliana China na India zinapaswa kuwa washirika

Rais wa China Xi Jinping akikutana na Waziri Mkuu wa India Narendra Modi katika wakati wa Mkutano wa 18 wa Viongozi wa BRICS mjini New Delhi, India, Septemba 12, 2026. (Xinhua/Wang Ye)
NEW DELHI - Rais wa China Xi Jinping na Waziri Mkuu wa India Narendra Modi wamefanya mazungumzo ya kubadilishana maoni kwa dhati na kwa kina, na kufikia maoni muhimu ya pamoja kwamba China na India zinapaswa kuwa washirika.
Viongozi hao wawili walikutana Jumamosi katika wakati wa Mkutano wa 18 wa Viongozi wa BRICS mjini New Delhi.
Xi amesema China siku zote imekuwa ikitendea na kuendeleza uhusiano wake na India kutoka mtazamo wa kimkakati wa juu na wa muda mrefu.
Xi amesema kuwa amekutana na Modi mara mbili katika miaka miwili iliyopita, na kuongoza uhusiano wa pande mbili kutoka mwanzo mpya hadi uboreshaji zaidi.
"Mawasiliano kati ya taasisi za nchi zetu mbili yamerudia tena katika hali ya kawaida hatua kwa hatua, orodha ya maeneo ya ushirikiano imeendelea kupanua, na biashara kati ya pande mbili imefikia rekodi mpya ya juu," Xi ameongeza.
Xi amesema, katika mazingira ya kimataifa yenye msukosuko, China na India zikiwa nchi mbili zenye idadi kubwa zaidi za watu duniani na nchi muhimu kati ya nchi za Kusini mwa Dunia, zinabeba majukumu muhimu.
Xi ametoa wito kwa pande hizo mbili kutilia maanani mustakabali wa binadamu na ustawi wa watu, kuhimiza kwa pamoja maendeleo yenye sifa bora zaidi ya ushirikiano wa BRICS, na kutoa mchango mkubwa zaidi kwa ajili ya amani, utulivu, maendeleo na ustawi wa duniani.
Pia amezihimiza China na India kuendeleza ushirikiano wa pande nyingi kwa msimamo wa ufunguaji mlango na jumuishi ili kuinufaisha dunia.
Kwa upande wake Modi amesema amefanya mikutano kadhaa yenye ufanisi na Xi, na kuongoza uhusiano wa India-China kuendelea kwa mwelekeo wa kuhimiza juhudi, hali ambayo inalingana na maslahi ya pamoja ya watu zaidi ya bilioni 2.8 wa nchi hizo mbili.
Amesema nchi mbili za India na China zenye ustaarabu mkubwa ulio wa maelfu ya miaka, zimefundishana kwa kupitia kubadilishana mawazo na kusonga mbele kwa pamoja.
"India siku zote inautendea na kuendeleza uhusiano wa India-China kutoka mtazamo wa kimkakati wa juu na wa muda mrefu, na inapenda kuwa mshirika wa China badala ya mshindani, na kuchukulia maendeleo ya kila upande kuwa ni fursa badala ya changamoto," ameeleza Modi.

Rais wa China Xi Jinping akikutana na Waziri Mkuu wa India Narendra Modi katika wakati wa Mkutano wa 18 wa Viongozi wa BRICS mjini New Delhi, India, Septemba 12, 2026. (Xinhua/Yan Yan)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



