Lugha Nyingine
Xi Jinping atoa wito wa kuzitaka nchi za BRICS kuwa na mshikamano na nchi za Kusini mwa Dunia na kuzidisha ushirikiano

Rais wa China Xi Jinping akitoa hotuba wakati akihudhuria kwenye Mkutano wa 18 wa Viongozi wa BRICS wa siku yake ya pili mjini New Delhi, India, Septemba 13, 2026. (Xinhua/Yan Yan)
NEW DELHI - Rais wa China Xi Jinping ametoa wito kwa nchi za BRICS kuimarisha mshikamano kati ya nchi za Kusini mwa Dunia na kufanya kazi nzuri za kuhimiza juhudi na kutuliza hali katika mambo ya dunia nzima.
Katika hotuba yake iliyotolewa kwenye mkutano wa viongozi wa BRICS wa siku yake ya pili mjini New Delhi jana Jumapili, Xi pia ametoa mapendekezo kuhusu mambo halisi ili kuimarisha zaidi ushirikiano wa nchi za BRICS ulio wa kuweka mkazo zaidi katika maeneo yanayoibukia ya AI, biashara, viwanda vya kidijitali na viwanda vya utengenezaji bidhaa.
Xi amesema kuwa wakati mabadiliko ambayo hayajawahi kutokea katika miaka 100 iliyopita yakiongezeka kwa kasi duniani kote, nchi za Kusini mwa Dunia zimekuwa zikijitokeza kwa pamoja, na kuwa msukumo muhimu kwa dunia ya ncha nyingi.
"Wakati huo huo, hali ya kimataifa inasukasuka bila kusita na inajaa hatari na changamoto," amesema Xi, na akiongeza kuwa, ili kuleta utulivu kwa dunia na kuifanya kuwa dunia nzuri zaidi, nchi za BRICS lazima zitumie fursa ya kihistoria, ziwe na mshikamano na nchi za Kusini mwa Dunia, na kusukuma mbele ustawi wa binadamu wote.
"Nchi za Kusini mwa Dunia zinapaswa kulinda kwa pamoja usimamizi kwa mujibu wa sheria katika mambo ya kimataifa, kulinda kanuni za kimsingi za uhusiano wa kimataifa kuhusu usawa wa mamlaka ya nchi, kutoingilia mambo ya ndani ya nchi nyingine, na kutatua migogoro kwa njia ya amani," amesema Xi.
Amesema ni lazima kuhakikisha kuwa sheria za kimataifa na kanuni za kimataifa zinatumika kwa watu wote, bila kuwa na vipimo viwili vya utekelezaji.

Waandishi wa habari wakifanya kazi kwenye kituo cha vyombo vya habari ndani ya Kituo cha Maonesho cha India ambapo ni ukumbi mkuu wa Mkutano wa 18 wa Viongozi wa BRICS mjini New Delhi, India, Septemba 12, 2026. (Xinhua/Javed Dar)
Xi amesema nchi za Kusini mwa Dunia zinapaswa pia kusukuma mbele kwa pamoja usimamizi wa usalama, kukabiliana na matishio dhidi ya usalama wa jadi na usio wa jadi, na kuboresha usimamizi wa tabianchi duniani.
Katika hotuba yake hiyo, Xi alitoa mapendekezo matano juu ya ushirikiano wa nchi za “BRICS kubwa zaidi” unaohusisha AI, biashara na uwekezaji, viwanda vya kidijitali, utengenezaji wa bidhaa kwa teknolojia ya AI, na kujiendeleza kwa vipaji katika sayansi na teknolojia.
“Ili kufanikisha mambo makubwa na kupata maendeleo makubwa, ni lazima kuimarisha msingi wa ushirikiano wa BRICS kubwa zaidi,” amesema Xi, akitoa wito wa kutumia uhusiano wa karibu wa nchi za BRICS na masoko mengine yanayojitokeza pamoja na nchi za Kusini mwa Dunia, kushikilia ufunguaji mlango na ushirikiano wa kunufaishana ili kupata maendeleo kwa pamoja, kuhakikisha utulivu na uendeshaji mzuri wa minyororo ya uzalishaji wa viwanda na utoaji wa bidhaa, na kukuza soko kubwa la utandawazi.

Mtembeleaji akiangalia mfano wa treni ya sabwe ya Xiamen kwenye maonyesho ya Mapinduzi Mapya ya Viwanda ya BRICS 2024, Xiamen, Mkoa wa Fujian, kusini-mashariki mwa China, tarehe 10 Septemba 2024.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



