Rais wa Senegal apokea mwenge wa Olimpiki ya Vijana kwa Michezo ya Dakar 2026

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Septemba 14, 2026

Rais wa Senegal Bassirou Diomaye Faye akitoa hotuba kwenye hafla ya kuupokea mwenge wa Olimpiki ya Vijana kwa ajili ya Michezo ya Olimpiki ya Vijana ya Dakar 2026 nje ya Ikulu ya Rais jijini Dakar, Senegal, tarehe 12 Septemba 2026. (Picha na Papa Demba Gueye/Xinhua)

DAKAR - Rais wa Senegal Bassirou Diomaye Faye amepokea mwenge wa Olimpiki ya Vijana kwa ajili ya Michezo ya Olimpiki ya Vijana ya Dakar 2026 kwenye hafla iliyofanyika nje ya Ikulu ya Rais katika mji mkuu wa Dakar siku ya Jumamosi.

Kwenye hafla hiyo, Faye alipokea mwenge huo kutoka kwa Mamadou Diagna Ndiaye, mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Michezo hiyo ya Dakar 2026. Rais wa Kamati ya Kimataifa ya Olimpiki, Kirsty Coventry, alihudhuria hafla hiyo pamoja na mamia ya vijana na wanamichezo.

Faye alisema kuwasili kwa mwenge huo kunaakisi imani ya jumuiya ya kimataifa kwa Senegal na kunaonyesha kuwa nchi hiyo hutimiza ahadi zake, huku vijana wake wakiwa rasilimali yake kuu.

"Mwenge huu unatuambia kuwa Afrika haitazami tu; Afrika inakaribisha," alisema, akiwahimiza vijana wa Senegal kuonyesha nguvu, ukarimu na azma yao wakati wa michezo hiyo.

"Taswira ambayo wageni wetu watabaki nayo ni ile mtakayowapa," alisema Faye, na kuongeza, "Ifanyeni Senegal ijivunie, na ifanyeni Afrika nzima ijivunie."

Ujumbe wa Senegal ulipokea mwenge huo siku ya Alhamisi wiki iliyopita kwenye hafla iliyofanyika katika Uwanja wa Panathenaic jijini Athens, Ugiriki.

Safari ya kukimbia na mwenge huo kwa kupokezana nchi nzima imepangwa kuanza leo Jumatatu ambapo utapitishwa katika mikoa yote 14 ya Senegal. Wabeba mwenge takribani 450, wakiwemo wanamichezo, vipaji vya vijana, wawakilishi wa mashirika ya kiraia na watu mashuhuri wa Senegal, wanatarajiwa kushiriki.

Michezo ya Olimpiki ya Vijana ya Dakar 2026 itafanyika kuanzia tarehe 31 Oktoba hadi 13 Novemba, ikileta pamoja wanamichezo takriban 2,700 watakaoshindana katika michezo 25. Hili litakuwa tukio la kwanza la michezo ya Olimpiki kufanyika katika bara la Afrika.

Rais wa Senegal Bassirou Diomaye Faye (katikati) akiwa ameshika mwenge kwenye hafla ya kuupokea mwenge wa Olimpiki ya Vijana kwa ajili ya Michezo ya Dakar 2026 nje ya Ikulu ya Rais jijini Dakar, Senegal, Septemba 12, 2026. (Picha na Papa Demba Gueye/Xinhua)

Rais wa Senegal Bassirou Diomaye Faye (wa pili, kutoka kushoto) akiwa ameshika mwenge kwenye hafla ya kuupokea mwenge wa Olimpiki ya Vijana kwa ajili ya Michezo ya Dakar 2026 nje ya Ikulu ya Rais jijini Dakar, Senegal, Septemba 12, 2026. (Picha na Papa Demba Gueye/Xinhua)

Rais wa Senegal Bassirou Diomaye Faye (kushoto) akipokea mwenge kutoka kwa Mamadou Diagna Ndiaye, mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Michezo ya Olimpiki ya Vijana ya Dakar 2026, kwenye hafla ya kuupokea mwenge wa michezo hiyo nje ya Ikulu ya Rais jijini Dakar, Senegal, Septemba 12, 2026. (Picha na Papa Demba Gueye/Xinhua)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha