Lugha Nyingine
Mkutano Mkuu wa IAEA wafunguliwa wakati kuna hofu inayoongezeka juu ya kuenea kwa silaha za nyuklia

Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Umoja wa Mataifa mjini Vienna, Bibi Monica Juma, akihutubia Mkutano Mkuu wa 70 wa Shirika la Kimataifa la Nishati ya Atomiki (IAEA) mjini Vienna, Austria, tarehe 14 Septemba 2026. (Xinhua/He Canling)
Mkutano Mkuu wa 70 wa Shirika la Kimataifa la Nishati ya Atomiki (IAEA) ulifunguliwa Jumatatu mjini Vienna, kukiwa na wito wa kuimarisha ushirikiano wa pande nyingi na kuwepo kwa juhudi za kudumisha usimamizi wa kimataifa wa kuzuia kuenea kwa silaha za nyuklia, katika wakati hali ya wasiwasi ya siasa za kijiografia inayozidi kuwa mbaya.
Mkurugenzi mkuu wa Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Vienna Bibi Monica Juma, ametoa ujumbe wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres, akisema mkutano huu unafanyika wakati dunia inakabiliana na msukosuko mkubwa na hali sintofahamu. Mashambulizi dhidi ya vituo vya nyuklia yanaongezeka, vichocheo vya kuenea kwa silaha za nyuklia vinaongezeka, huku njia za kudhibiti zikiendelea kupungua.
Mkurugenzi Mkuu wa IAEA Bw. Rafael Grossi amesema kwenye mkutano huo kuwa Mkataba wa Kuzuia Kuenea kwa Silaha za Nyuklia (NPT) unaendelea kuwa msingi wa usimamizi wa kimataifa wa kuzuia kuenea kwa silaha za nyuklia.

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Kimataifa la Nishati ya Atomiki (IAEA), Rafael Grossi, akizungumza kwenye Mkutano Mkuu wa 70 wa IAEA mjini Vienna, Austria, tarehe 14 Septemba 2026. (Xinhua/He Canling)

Watu wanahudhuria Mkutano Mkuu wa 70 wa Shirika la Kimataifa la Nishati ya Atomiki (IAEA) mjini Vienna, Austria, tarehe 14 Septemba 2026. (Xinhua/He Canling)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



