Xi awahimiza polisi wa China kuendelea kujitolea kuwahudumia wananchi kwa uwajibikaji na moyo wa kujitoa

(CRI Online) Septemba 16, 2026

Rais Xi Jinping wa China amewataka maafisa wa polisi nchini kuendelea kujitolea kuwahudumia wananchi, kuwa walinzi waaminifu wa Chama na wananchi, na kuonyesha moyo thabiti wa uwajibikaji na kujituma kikazi.

Xi, ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China na Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi ya China, alitoa kauli hiyo alipojibu barua ya polisi wa mtaani mjini Zhangzhou, mkoani Fujian, Mashariki mwa China.

Katika barua yake kwa kitengo cha polisi cha "Zhangzhou 110", Xi aliwapongeza maafisa wake kwa kujitolea na kufanya kazi kwa bidii katika mitaa ili kuwahudumia wananchi na kudumisha utulivu wa kijamii.

Kitengo cha "Zhangzhou 110" ni kimojawapo cha vitengo vya mtaani vya jeshi la polisi la China vilivyo mfano wa kuigwa. Tokea mwaka 1990, kimeanzisha na kuendeleza mfumo wa mwitikio wa haraka unaoambatana na huduma ya simu ya dharura ya polisi ya nambari 110, kikichukua nafasi muhimu katika kupambana na uhalifu, kudumisha usalama wa umma, na kuhudumia jamii.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha