Kutoka Kibera hadi kuwa kati ya nafasi 15 bora duniani: Mwanafunzi wa Kenya aweka historia katika shindano la lugha ya Kichina

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Septemba 16, 2026

Mwalimu wa lugha ya Kichina Meng Lingyao (wa 3 kulia) akimwelekeza Miriam Achieng Kenyatta (wa pili kushoto) wakati wa darasa la lugha ya Kichina katika Chuo cha Confucius katika Chuo Kikuu cha Nairobi, Kenya, Septemba 8, 2026. (Xinhua/Xie Jianfei)

Miriam Achieng Kenyatta, mwanafunzi wa uhandisi wa kijiografia mwenye umri wa miaka 23 katika Chuo Kikuu cha Nairobi, alipata mapokezi mazuri aliporudi nyumbani baada ya kuandika historia kwenye Shindano la 25 la Ustadi wa Lugha ya Kichina la "Daraja la Kichina" kwa Wanafunzi wa vyuo vya nchi mbalimbali za nje ya China.

Bi. Miriam ambaye amekulia katika eneo la makazi yasiyo rasmi la Kibera jijini Nairobi, maisha yake yalibadilishwa kutokana na udadisi aliokuwa nao tangu utotoni uliochochewa na filamu moja ya televisheni. Shauku yake ilimletea mafanikio makubwa zaidi kuwahi kufikiwa na Mkenya kwenye shindano la kimataifa la uhodari wa lugha ya kichina, ambapo alichaguliwa kuwa miongoni mwa wanafunzi bora 15 duniani kote.

Miriam Achieng Kenyatta akiwa kwenye picha wakati wa fainali za kimataifa za Shindano la 25 la Ustadi wa Lugha ya Kichina la "Daraja la Kichina" kwa wanafunzi wa vyuo vikuu kutoka nchi mbalimbali za nje ya China, lililofanyika mjini Xiamen, Fujian tarehe 23 Agosti 2026. (Xinhua)

(Wahariri wa tovuti:Liu Mengxue,Zhao Jian)

Picha