Lugha Nyingine
TikTok na ICC zazindua maabara za kidijitali za kibiashara kuboresha biashara ya mtandaoni kwa kampuni ndogo na za kati
Kampuni ya TikTok na Shirikisho la Kimataifa la Wafanyabiashara (ICC) jumanne wiki hii zimezindua maabara ya kijitali ya biashara jijini Accra, Ghana, kwa lengo la kuwezesha wafanyabiashara wadogo ujuzi wa kidijitali na vifaa.
Pendekezo hilo la kimataifa linalolenga kufungua fursa za biashara ya kidijitali kwa wafanyabiashara wadogo katika masoko yaliyochaguliwa katika maeneo ya Latin America, Afrika, na Asia Kusini Mashariki, pia litawezesha biashara ndogo kufikia soko kubwa, kuongeza kipato, na kujenga unyumbufu wa muda mrefu.
Akizungumza kwenye uzinduzi huo, mkuu wa Uhusiano wa Serikali na Sera za Umma wa TikTok kanda ya Kusini mwa Afrika, Tholoana Ncheke-Mahlaela amesema, lengo ni kupunguza vizuizi vya upatikanaji katika kuingia na kuwasiliana kwa wafanyabiashara na wateja mbali zaidi ya jamii zao za karibu.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



