Huku zikiwa zimebaki siku chini ya 30 kabla ya kufunguliwa kwa Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi ya Beijing, baadhi ya waandishi wa habari wameonekana katika kituo cha vyombo vya habari cha michezo hiyo wakibeba mikoba ya Michezo ya Olimpiki ya Majira ya joto ya Beijing 2008 ambayo waandishi wa habari walipewa bure. Mpiga picha wa Iran alisema anabeba mkoba huo kila akipiga picha kwenye mashindano ya michezo.
Zhang amekusanya na kuhifadhii vitu zaidi ya 5000 kuhusu Michezo ya Olimpiki, vikiwemo bendera za Michezo ya Olimpiki, vitu vya baraka, myenge n.k.
“Sikuweza kushiriki kwenye Michezo ya Olimipiki. Ninatumai kwamba wachezaji wa China wanaovaa viatu vya kuteleza kwenye barafu ninavyotengeneza wataleta medali za dhahabu nyumbani” anasema Wang Yang, mtengenezaji wa viatu vya kuteleza kwenye barafu, ambaye aliwahi kuwa mchezaji wa mbio za kuteleza kwa kasi katika mduara mfupi kwenye barafu.
TEHERAN- Huku Michezo ya Olimpiki ya Majira ya baridi ya Beijing ikikaribia, wanamichezo wa Iran wa kuteleza kwa kasi kwenye milima ya theluji ya Alpine wanawania nafasi ya kushindana kwenye jukwaa kubwa zaidi la michezo mjini Beijing. "Natumai nitaweza kufuzu kwa Michezo ya Olimpiki ya Majira ya baridi ya Beijing na ningependa sana kwenda China," anasema Fatemeh Kia Shemshaki mwenye umri wa miaka 17, mwanamichezo wa alpine ambaye anashiriki katika mashindano yanayoendelea ya kufuzu kwa Michezo ya Olimpiki huko Iran kwenye Uwanja wa Kuteleza kwenye theluji wa Hoteli ya Darbandsar.