Aliyekuwa Mchezaji Aanzisha Kampuni kutengeneza Viatu vya Kuteleza kwenye Barafu kwa wa Wanariadha wa kulipwa wa China

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Januari 19, 2022
Aliyekuwa Mchezaji Aanzisha Kampuni kutengeneza Viatu vya Kuteleza kwenye Barafu kwa wa Wanariadha wa kulipwa wa China
Wang Yang akichunguza soli ya viatu yenye makali kwa ajili ya kuteleza kwenye barafu. (Picha/Chinanews.com)

“Sikuweza kushiriki kwenye Michezo ya Olimipiki. Ninatumai kwamba wachezaji wa China wanaovaa viatu vya kuteleza kwenye barafu ninavyotengeneza wataleta medali za dhahabu nyumbani” anasema Wang Yang, mtengenezaji wa viatu vya kuteleza kwenye barafu, ambaye aliwahi kuwa mchezaji wa mbio za kuteleza kwa kasi katika mduara mfupi kwenye barafu.

Wang Yang aliyezaliwa Mwaka 1983 alianza kujifunza michezo ya kuteleza kwenye barafu akiwa na umri wa miaka 7. Mnamo Mwaka 2001, alianza kuwa wanariadha wa kulipwa wa mchezo wa kuteleza kwenye barafu katika Mji wa Changchun, Mkoa wa Jilin, Kaskazini Mashariki mwa China. Baada ya miaka minne, wakati akijiandaa kwa kushiriki kwenye Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi ya Torino baada ya kuteuliwa kujiunga na Timu ya Taifa ya China, kwa bahati mbaya Wang alipata majeraha hali ambayo ilimlazimu kustaafu mapema.

Baada ya kustaafu, Wang Yang alikuja na wazo la kutengeneza viatu vya kuteleza kwenye barafu maalum kwa ajili ya wachezaji wa China. “Nilipokuwa mchezaji niliwahi kujaribu kutumia viatu vya chapa nyingi za nchi za kigeni, lakini nilibaini havifai kwa maumbo ya miguu ya Wachina” anasema Wang Yang.

Ili kuweka wazo lake katika utekelezaji, Wang alikusanya data husika kwenye mtandao wa intaneti, akajifunza mchakato wa kutengeneza viatu vya kuteleza kwenye barafu, kisha akanunua cherehani kwa ajili kuboresha ufundi wake wa kushona.

Mnamo Mwaka 2010, Wang Yang alitumia karibu akiba yake yote ya fedha kulipa malipo ya awali kununua chapa ya Australia ya viatu vya kuteleza kwenye barafu. Baada ya ununuzi huo, Wang Yang alikuwa akilala saa nne au tano tu kila siku, akijitahidi kujifunza ufundi maalum wa kutengeneza viatu vya kuteleza kwenye barafu.

Mwishowe jitihada za Wang zimemlipa, viatu vyake vya kuteleza kwenye barafu alivyotengeneza kwa ajili ya Mchezaji wa Timu ya Taifa ya Olimpiki ya China Zhang Hong vilimsaidia Zhang kushinda medali ya dhahabu ya kwanza ya China ya mbio za kuteleza kwa kasi kwenye barafu katika Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi ya Sochi 2014.

Hivi sasa Bw. Wang anaendesha kiwanda cha kutengeneza viatu chenye eneo la ukubwa wa mita za mraba zaidi ya 3000, kiwanda hicho kimepanuka kutoka kwenye karakana ndogo yenye mita za mraba 50 tu. Kiwanda hicho kinazalisha viatu 10,000 hivi vya kuteleza kwenye barafu, vikiwemo viatu 500 vinavyotengenezwa maalum kwa ajili ya wanariadha wa kulipwa .

Viatu vilivyotengenezwa na Bw. Wang siyo tu vimejulikana zaidi umaarufu nchini China, bali pia vinauzwa katika nchi za Uholanzi, Ufaransa, Uingereza, Ubelgiji, Austria, Russia, Japan, Korea ya Kusini na nchi nyingine kadha wa kadha.

Kwa kuwa Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi ya Beijing 2022 itawadia, katika majira ya joto ya mwaka 2021, Wang Yang aliacha kwa muda kazi ya kutengeneza viatu vya wachezaji wa kawaida, na kujikita zaidi katika utengenezaji wa viatu vya wachezaji wa kuteleza kwenye barafu watakaoshiriki kwenye Michezo hiyo ya Olimpiki.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha