Baadhi ya wanafunzi wa Kenya wanaosoma Chuo Kikuu cha Jiaotong cha Beijing, China ambao hapo awali walimwandikia barua Rais Xi Jinping wa China na kupokea jibu lake wameeleza kuwa reli ya SGR ya Mombasa-Nairobi iliyojengwa na Shirika la Madaraja la China imeleta mageuzi makubwa katika sekta za uchumi na usafirishaji nchini Kenya. Wanafunzi hao walimwandikia barua Rais Xi mwezi Oktoba mwaka jana baada ya kumaliza masomo yao katika chuo hicho, wakieleza shukrani zao kwake kwa kuja na Pendekezo la Ukanda Mmoja, Njia Moja ambalo limeleta manufaa makubwa kwa watu na nchi mbalimbali duniani ikiwemo Kenya ambayo imenufaika na miradi ya ushirikiano wa pande mbili ikiwemo miundombinu hususan reli hiyo ya SGR ya Nairobi-Mombasa ambako wanafanya kazi na fursa za ufadhili wa masomo ambazo wao ni moja ya wanufaika.
Rais wa Comoro Bw. Azali Assoumani amesema, katika ushirikiano na nchi za Afrika, China siku zote imekuwa ikifuata kanuni za kutendeana kwa usawa na kushirikiana kwa mafanikio bila kujali ukubwa wa nchi, jambo ambalo limeweka msingi wa ushirikiano kati ya nchi za 'Dunia ya Kusini' na kuwezesha kujenga dunia ya haki ambayo maslahi ya pande zote yanalindwa.
Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) Felix Tshisekedi (mbele katikati) (Xinhua/Shi Yu) Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) Felix Tshisekedi amesema China imedhihirishwa kuwa ni mwenzi wa kutegemeka katika maendeleo ya bara la Afrika. Akizungumza siku chache kabla ya kuhudhuria mkutano wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC) unaofanyika hapa Beijing, Rais Tshisekedi amesema, chini ya mifumo kama FOCAC, miradi mingi ya ushirikiano imetekelezwa nchini DRC, na kutolea mfano mradi wa bandari kavu ya Sakania, kituo cha kuzalisha umeme cha Busanga, na kituo kidogo cha Kinsuka.
Mkutano wa Kilele wa 2024 wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC) utafanyika kuanzia kesho Jumatano mjini Beijing na Katibu Mtendaji wa Kamisheni ya Kiswahili ya Afrika Mashariki Dkt. Caroline Asiimwe amesema kuwa, mabadiliano na ushirikiano wa nyanja ya lugha kati ya China na Afrika yanasaidia kuunganisha mawasiliano ya watu kati ya pande hizo mbili.