Kazan ni mji mkuu wa Jamhuri ya Tatarstan ambayo iko chini ya Shirikisho la Russia. Kuna maeneo mengi ya kupendeza katika mji huu, maarufu zaidi miongoni mwa maeneo hayo ni Kazan Kremlin.
"China inafanya kazi muhimu katika kuhimiza kukamilisha mfumo wa ushirikiano wa BRICS siku hadi siku, kutetea usawa na haki na ushirikiano wa pande nyingi. Kazi ya uongozi ya China inahimiza kuendeleza mfumo wa ushirikiano kati ya nchi za BRICS.
Mkurugenzi wa Ofisi ya mambo ya nje ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China Bw. Wang Yi hivi karibuni alisema, China inakaribisha washiriki wengi zaidi wenye nia moja kutoka nchi za Kusini kujiunga na familia ya BRICS.
Mkurugenzi wa Ofisi ya Kamati ya mambo ya nje ya China, Bw. Wang Yi Jumatano alitoa wito kwa nchi za BRICS kushikana mikono katika kushughulikia matishio dhidi ya usalama katika mkutano wa ngazi ya juu.