Rais Xi Jinping wa China amekutana na mwenzake wa Misri Abdel Fattah El-Sisi Jumatano usiku pembezoni mwa Mkutano wa 16 wa Viongozi wa nchi za BRICS uliofanyika mjini Kazan, Russia. Rais Xi ameipongeza na kuikaribisha Misri kushiriki kwa mara ya kwanza katika mkutano huo wa viongozi wa nchi za BRICS kama mwanachama rasmi.
Rais Xi Jinping wa China akikutana na Waziri Mkuu wa India Narendra Modi katika wakati wa Mkutano wa 16 wa Viongozi wa BRICS huko Kazan, Russia, Oktoba 23, 2024. (Xinhua/Shen Hong) KAZAN, Russia - Rais Xi Jinping wa China jana Jumatano alipokutana na Waziri Mkuu wa India Narendra Modi katika wakati wa Mkutano wa 16 wa Viongozi wa nchi za BRICS alitaka China na India kuimarisha mawasiliano na ushirikiano, kuongeza hali ya kuaminiana kimkakati, na kuhimizana katika kutafuta matarajio ya maendeleo.
KAZAN, Russia - Viongozi wa nchi za BRICS wametoa taarifa ya pamoja inayohusu masuala mbalimbali kuanzia mageuzi ya Umoja wa Mataifa (UN) hadi migogoro inayoendelea duniani, kufuatia mkutano wa viongozi wa kundi hilo uliofanyika Jumatano mjini Kazan ambapo taarifa hiyo inajumuisha vipengele 134 kwa jumla. "Tunasisitiza tena kuunga mkono mageuzi ya Umoja wa Mataifa katika pande zote, ikiwa ni pamoja na Baraza lake la Usalama, kwa nia ya kuufanya kuwa wa kidemokrasia, wakilishi, wenye mchango na fanisi," taarifa hiyo inasema.
Rais Xi Jinping wa China akihutubia Mkutano wa 16 wa Viongozi wa nchi za BRICS huko Kazan, Russia, Oktoba 23, 2024. Mkutano huo umeandaliwa na Rais wa Russia Vladimir Putin, na kuhudhuriwa na Rais wa China Xi Jinping, Rais wa Brazil Luiz Inacio Lula da Silva (kwa njia ya video), Rais wa Misri Abdel-Fattah al-Sisi, Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed, Waziri Mkuu wa India Narendra Modi, Rais wa Iran Masoud Pezeshkian, Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa na Rais wa Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) Sheikh Mohamed bin Zayed Al Nahyan.