Rais wa China Xi Jinping akikutana na Rais wa Russia Vladimir Putin huko Kazan, Russia, Oktoba 22, 2024. (Xinhua/Ding Haitao) KAZAN, Russia - Rais wa China Xi Jinping jana siku ya Jumanne alipokutana na Rais wa Russia Vladimir Putin alisema kuwa China na Russia zimepata njia sahihi ya kuwa na ujirani mwema kwa nchi kubwa jirani, njia hiyo ni kutofungamana na upande wowote, kutopambana na kutolenga upande wowote wa tatu.
KAZAN, Russia - Rais wa China Xi Jinping amewasili Kazan, Russia jana Jumanne kwa kuhudhuria Mkutano wa 16 wa Wakuu wa nchi za BRICS, ambapo maofisa wa Russia walimlaki Rais Xi kwenye uwanja wa ndege huku askari wa gwaride la heshima wakiwa wamejipanga pande zote za zulia jekundu kumpa heshima kiongozi huyo wa China, na vijana wa Russia waliokuwa wamevalia mavazi ya makabila wakimkaribisha kwa desturi na mila. Aidha, ndege ya kivita ya Russia ilionekana ikisindikiza ndege iliyokuwa imembeba Rais Xi.
BEIJING - Rais wa China Xi Jinping leo Jummane ameondoka Beijing kwa ajili ya kuhudhuria Mkutano wa 16 wa Viongozi wa BRICS utakaofanyika Kazan, Russia kutokana na mwaliko wa Rais wa Shirikisho la Russia Vladimir Putin. Watu wanaoambatana na Rais Xi katika safari hii ni Cai Qi, mjumbe wa kudumu wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) ambaye pia ni Mkurugenzi wa Ofisi Kuu ya Kamati Kuu ya CPC, na Wang Yi, Mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya CPC ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Nje wa China.
Washiriki wa Baraza la BRICS juu ya Ushirikiano kuhusu Mapinduzi Mapya ya Viwanda 2024 wakiwa kwenye picha ya kundi mjini Xiamen, Mkoa wa Fujian, kusini mashariki mwa China, Septemba 10, 2024. (Xinhua/Lin Shanchuan) MOSCOW - Ushirikiano uliopanuliwa wa BRICS utatoa mchango mkubwa zaidi katika kuboresha mfumo wa usimamizi wa dunia, amesema Balozi wa China nchini Russia Zhang Hanhui katika mahojiano maalum na Shirika la Habari la China, Xinhua kabla ya Mkutano wa 16 wa Viongozi wa BRICS uliopangwa kuanza leo Oktoba 22 hadi 24 mjini Kazan, Russia akisema kuwa mkutano huo ni wa kwanza kwa viongozi wa BRICS kufanyika nje ya mtandao tangu upanuzi wa kundi hilo.