人民网首页

Habari

Rais Xi asema ziara yake kupeleka uhusiano wa wenzi wa ushirikiano wa kimkakati kati ya China na Peru kwenye ngazi mpya

Rais wa China Xi Jinping akikaribishwa kwa furaha na Waziri Mkuu wa Peru Gustavo Adrianzen na maofisa wengine waandamizi baada ya kufika kwenye Uwanja wa Ndege wa Kijeshi wa Callao huko Lima, Peru, Novemba 14, 2024. (Xinhua/Li Xueren) LIMA - Rais Xi Jinping wa China amesema Alhamisi kwamba anaamini kwa juhudi za pamoja za pande zote mbili, ziara yake hii itapeleka uhusiano wa wenzi wa ushirikiano wa kimkakati wa China na Peru kwenye kiwango kipya, kuhimiza ushirikiano kati yao kupata matokeo halisi katika setka mbalimbali.

Marais wa China na Peru wahudhuria hafla ya kuzinduliwa kwa bandari ya Chancay

(Picha/Xinhua) Rais Xi Jinping wa China na Rais Dina Boluarte wa Peru wamehudhuria kwa pamoja hafla ya uzinduzi wa Bandari ya Chancay kwa njia ya video jana Alhamisi mjini Lima, Peru. Akizungumza kwenye hafla hiyo, Rais Xi amesema bandari hiyo ya Chancay italeta faida kubwa kwa Peru na kutoa nafasi nyingi za ajira.

(Picha/Xinhua)

Rais wa Peru aandaa hafla kubwa ya ukaribisho wa Rais Xi Jinping wa China

Rais Xi Jinping wa China siku ya Alhamisi alihudhuria hafla kubwa ya ukaribisho iliyoandaliwa na Rais Dina Boluarte wa Peru. Rais Xi aliwasili Peru mapema siku hiyo ili kufanya ziara ya kiserikali katika nchi hiyo na kuhudhuria Mkutano wa 31 wa Viongozi wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiuchumi ya Asia Pasifiki (APEC).

Xi Jinping achapisha makala aliyoandika na kuitia saini katika chombo cha habari cha Peru

Rais Xi Jinping wa China ambaye yupo kwenye ziara ya kiserikali mjini Lima nchini Peru na kuhudhuria Mkutano wa 31 wa Viongozi wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiuchumi ya Asia Pasifiki (APEC), siku ya Alhamisi amechapisha makala aliyoiandika na kuitia saini yenye kichwa "Acha Meli ya Urafiki kati ya China na Peru Ianze Safari" kwenye gazeti la El Peruano la Peru.

Iliyopita5 6 7 8 9 Inayofuata